Staa wa Nigeria Davido kuongoza Raha Fest katika bustani ya Uhuru Gardens [Maelezo]

Davido atakuwa kinara wa tamasha hilo la siku mbili litakalofanyika Machi 30 na Machi 31, 2024

Muhtasari

•Mwimbaji  kutoka Nigeria, Davido ataongoza tamasha la mwaka huu la Raha katika bustani ya Uhuru Gardens, Nairobi.

• Tikiti za Raha Fest sasa zinapatikana kwenye Ticket Yetu.

Davido
Image: HISANI

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nigeria David Adeleke almaarufu Davido ataongoza tamasha la mwaka huu la Raha katika bustani ya Uhuru Gardens, Nairobi.

Davido atakuwa kinara wa tamasha hilo la siku mbili litakalofanyika Machi 30 na Machi 31, 2024. Atakuwa akishiriki jukwaa na King Promise wa Ghana na gwiji wa amapiano wa Afrika Kusini Musa Keys na mastaa kadhaa wa Kenya.

Tamasha hilo pia linajumuisha safu ya kipekee ya vipaji vya Kenya na wasanii mashuhuri wa Kiafrika, akiwemo Sanaipei Tande, Samidoh, Nadia Mukami, Hart the Band, Nviiri the Storyteller, Femi One, Otile Brown, na nguli wa Kongo JB Mpiana.

 Tikiti za Raha Fest sasa zinapatikana kwenye Ticket Yetu.

 RAHA Fest inaahidi kuwa tajriba ya kipekee, inayowaleta pamoja wapenzi wa muziki kutoka nyanja mbalimbali ili kusherehekea utofauti wa muziki wa Kiafrika.

 "Tunafuraha kuleta Raha Fest kwenye bustani ya Uhuru na kutoa jukwaa ambalo linasherehekea uchangamfu na ubunifu wa muziki wa Kiafrika, sanaa na mitindo," waandaaji wa Raha Fest walisema.

"Tamasha hili sio tu la kusherehekea urithi wa kitamaduni bali pia ni uthibitisho wa utajiri wa sherehe za Kiafrika ambazo huchangia uzoefu wa tamasha la kimataifa."

Raha Fest ilimtangaza Zuri Health kwa fahari kuwa Mshirika rasmi wa Afya wa tamasha hilo, ikianzisha mtazamo wa afya njema kwa sherehe ya mwaka huu.

Zaidi ya hayo, Radio Africa inatumika kama mshirika rasmi wa vyombo vya habari, kueneza neno na msisimko kuhusu tamasha hilo kupitia redio na magazeti kwa hadhira pana.

Tikiti za Raha Fest sasa zinapatikana katika Tiketi Sasa na Ticket Yetu, na kuwapa watakaohudhuria fursa ya kujisajili katika sherehe hii isiyosahaulika ya muziki, sanaa na utamaduni wa Kiafrika.

Image: RAHA FEST