Pasta aliyemfukuza muumini madhabahuni kwa kudai ushuhuda wake ni feki ajutia kitendo chake

Pasta huyo alimuaibisha hadharani na kumwambia haonekani kama mhitimu wa Sheria, akienda kwa jinsi alivyozungumza. Pia alimwambia kwamba hakuna kitu kama “Bsc in Law” na akamtaka aondoke kwenye madhabahu.

Muhtasari

• "Mchungaji Mkuu anabakia kuwa na shauku sana na tayari amemfikia.”

• Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Katibu wa mchungaji mkuu Sylvester Edoh, ilisisitiza kwamba aibu hiyo haikukusudiwa na ni majibu ya papo kwa papo.

Mchungaji Paul Enenche
Mchungaji Paul Enenche
Image: FACEBOOK//Dunamis International Gospel Centre

Kanisa la Dunamis International Gospel Centre nchini Nigeria wamevunja kimya kwa kutoa taarifa kuhusiana na tukio la ‘aibu’ lililojiri kaitka ibada ya Jumapili kumhusisha mchungaji mkuu na muumini wa kike.

Kwa mujibu wa taarifa katika ukurasa wa Instagram wa kanisa hilo, walisema kwamba mchungaji mkuu Pau Enenche hakukusudia kumdhalilisha muumini huyo, Anyim Veronica kwa kupuuzilia mbali ushuhuda wake kuwa ni mhitimu wa digrii kitivo cha uanasheria.

Kisa hicho cha Jumapiliambacho kilivutia maoni mbalimbali wengi wakimkosoa mchungaji kwa kumzima muumini kutoendelea na ushuhuda wake akidai ni feki.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Katibu wa mchungaji mkuu Sylvester Edoh, ilisisitiza kwamba aibu hiyo haikukusudiwa na ni majibu ya papo kwa papo.

Inasomeka kwa sehemu:

"Lazima ielezwe wazi hapa kwamba kumwaibisha mtoa ushuhuda hadharani na mbele ya macho ya vyombo vya habari hakujakusudiwa kamwe; chochote kilichotokea kilikuwa chini ya msukumo wa wakati huo.”

“Kitendo cha Mchungaji Mkuu kiliegemezwa zaidi kwenye dhana yake na ya kanisa kwa kuonekana kuwa mtu wa wastani na sura yoyote ya uwongo.”

"Ingawa tunasalia thabiti katika shauku yetu ya ubora, kutovumilia ujinga na uwongo, tunataka kusisitiza ukweli kwamba hakuna madhara au uchungu uliowahi kudhamiriwa na Mchungaji Mkuu dhidi ya Bi. Anyim Veronica Nnenna. Mchungaji Mkuu anabakia kuwa na shauku sana na tayari amemfikia.”

“Kama Tume, tunajutia kila usumbufu, maudhi na aibu ambayo hali hii mbaya imemsababishia Bi. Anyim Veronica Nnenna. Tunasalia kujitolea kwa ustawi wake wa kimwili na ukuaji wake wa kiroho.”

Hapo awali Radiojambo.co.ke iliripoti kwamba video iliyosambazwa kwa njia ya mtandao ilionyesha Mchungaji Enenche akimkashifu mtoa ushuhuda kwa madai yake ya kuwa mhitimu wa kwanza katika familia yake.

Mwanamke huyo, Anyim Vera, ambaye alidai kuwa alihitimu na "Bsc katika Sheria" kutoka Chuo Kikuu Huria cha Kitaifa cha Nigeria, alikatishwa na Enenche, ambaye alimshutumu kwa kusema uwongo.

Alimwambia haonekani kama mhitimu wa Sheria, akienda kwa jinsi alivyozungumza. Pia alimwambia kwamba hakuna kitu kama “Bsc in Law” na akamtaka aondoke kwenye madhabahu.

Watumizi wa mitandao ya walionyesha kughadhabishwa kwa namna ambayo Mchungaji Enenche alihutubia Anyim, wakitaka kuomba msamaha.