Rapa Khaligraph Jones amezungumzia safari ya ufanisi wake kimuziki na kufichua kwamba shoo yake ya kwanza kutumbuiza alilipwa shilingi elfu 50 pesa taslimu.
Jones katika mahojiano na Oga Obinna alieleza kwamba shoo ya kwanza aliitwa kutumbuiza katika chuo cha Zetech ambapo baada ya shoo alikabidhiwa bunda na noti shilingi 50.
Msanii huyo alichora taswira ya jinsi alivyopokea hela hizo ambazo kwake zilikuwa ni hela ndefu sana iizingatiwa kwamba ndio mwanzo alikuwa anachipukia.
Hakuweza kulala usiku kucha akiwa na elfu 50 mfukoni katika kochi la sebule ya mama yake.
“Shoo yangu ya kwanza nililipwa elfu 50 ghafla, ilikuwa ni Zetech, waliniita wakaniambia tunataka utumbuize. Tukimalzia kutumbuiza nikaambia huyo jamaa sasa si unilipe, jamaa alinitolea pesa nyingine sijawahi ona. Huo wakati maisha yalikuwa yamenichapa hadi nikahama kutoka Dandora nikarudi kwa mama yangu. Nilikuwa nalala katika kochi sebuleni kwa mamangu kwa sababu nyumba ilikuwa ya chumba kimoja cha kulala,” Jones alisema.
“Alinipatia nikaingiza kwa mfuko ulikuwa umefura, sikuambia kwanza mtu. Alinihesabia 50k nikiangalia hivi. Nilifika kwa mama usiku nilikaa kwa kiti mpaka asubuhi mfuko wangu ulikuwa umefura, siamini,” aliongeza.
Asubuhi yake, aliamua kutafuta uhuru wake kwa kujiondoa katika nyumba ya mamake na kujianzishia maisha huku.
“Asubuhi nimeamka kama nimetafuta kanyumba nikampa mama kitu kidogo pia kwa sababu mamangu amekuwa mtu wangu wa maombi muda wote, nikajipangishia maisha huo mwaka wa 2012,” Khaligraph alisema.
Kabla ya kupata ufanisi huo, alisema kwamba mwaka 2012 alikuwa anaishi na yeye na baadae baba akatoka na kurudi nyumbani ambapo baadae alifariki, huo ndo ulikuwa wakati mgumu sana kwake.
Huo wakati kwa mujibu wa Jones, alihisi kuachia muziki kwani mwaka mmoja nyuma pia alikuwa ameshtakiwa mahakamani na jamaa mmoja aliyemsingizia kwamba amemuibia.
Alikaa rumande kwa kipindi cha wiki tatu.