logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Willy Paul awalilia wanahabari kuwahi nyumbani kwake kwa haraka kisa hofu ya polisi

“Hii ni dharura, kama unajua nyumbani kwangu tafadhali kimbia." Pozee alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 March 2024 - 09:54

Muhtasari


  • • Aliwataka watu wote haswa waandishi wa habari kulichukulia jambo hilo kuwa la dharura na kuwahi nyumbani kwake.
  • • “Hii ni dharura, kama unajua nyumbani kwangu tafadhali kimbia. Waandishi wote wa habari… wanataka kuniondoa,” Pozee alisema bila kutoa taarifa Zaidi.
  •  
Willy Paul

Msanii wa kizazi kipya, Willy Paul asubuhi ya Jumatatu alitoa ombi kwa wanahabari na waandishi wa habari wote kuwahi nyumbani kwake kwa kile alidai kwamba boma lake lilikuwa limezingiwa na watu wanaodhaniwa kuwa maafisa wa polisi.

Kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii, Pozee kama anavyojiita, alidai kwamba watu hao walioko katika sare za polisi walikuwa wamezingira nyumba yake kwa lengo la kutaka kumtia mbarano.

Mkali huyo wa ‘Keroro’ aliwaomba waandishi wa habari kuwahi ili kunasa tukio zima, akisema kwamba hii si mara ya kwanza polisi wanazingira nyumba yake kwa lengo la kumkamata.

Alisema kwamba aliarifiwa polisi wapo langoni pake wakitaka kumkamata kwa kile inadaiwa alimgonga mtu na gari lake kisa kutoweka sehemu ya tukio.

“Nimearifiwa kwamba kuna maafisa wa polisi nje ya nyumba yangu Syotani Villas wananisubiri wakisema niligonga mtu na gari langu kisa nikatoroka. Wanataka kuniua. Jambo sawia na hili lilitokea mwaka jana. Kama jambo lolote litatokea kwangu basi mjue ni watu walioko katika sare za polisi na wako nje ya nyumba yangu sasa hivi,” Willy Paul aliandika.

Aliwataka watu wote haswa waandishi wa habari kulichukulia jambo hilo kuwa la dharura na kuwahi nyumbani kwake.

“Hii ni dharura, kama unajua nyumbani kwangu tafadhali kimbia. Waandishi wote wa habari… wanataka kuniondoa,” Pozee alisema bila kutoa taarifa Zaidi.

Hata hivyo, baadhi walichukulia jambo hilo kimasihara wakisema kwamba pengine ameita waandishi wa habari ili kutoa tangazo la ujio wa ngoma yake au kitu kingine.

Wengine pia walimtania kwamba ni jamaa muoga ambaye hataki kutoka ili kujua kwa undani mbona polisi wanamtaka kama kweli ana uhakika hakutekeleza ajali aliyoitaja.

“Jina la jam mpya?” Dj Amm alimuuliza.

“Kumbe unakuanga mwoga 😂😂😂 ni mm na maboyz wangu tuko hapo 😂😂” dural.8

“Ama ni kaligraph anashoot vida hapo njee na hujui😂” gaspop9

“Ni polisi wanawake, wewe wakune wasikie utamu wa keroro Mr Mkunaji😂” grandsun.m


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved