logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mauaji ya ‘Sniper’, DPP apendekeza mashtaka ya mauaji dhidi ya washukiwa

Uchunguzi wa mwili wa marehemu ulibaini kuwa alifariki kwa kunyongwa.

image
na Davis Ojiambo

Habari19 January 2024 - 06:50

Muhtasari


  • • Mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor, aliyefanya uchunguzi huo, alisema Sniper alikuwa na alama kwenye shingo yake na alionyesha dalili za mtu aliyekosa oksijeni.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) amependekeza washukiwa wawili kushtakiwa kwa mauaji ya mwanablogu Daniel Muthiani Bernard almaarufu Sniper katika kaunti ya Meru.  

Katika taarifa DPP alisema kuna ushahidi wa kutosha kuendeleza mashtaka ya mauaji dhidi ya Vincent Muriithi Kirimi almaarufu Supuu na Murangiri Kenneth Guantai almaarufu Tali.

‘Sniper’ alitoweka Desemba 2 mwaka jana kabla ya mwili wake kugunduliwa wiki mbili baadaye.

Washukiwa watano baadaye walikamatwa kuhusiana na mauaji hayo. Walijumuisha; Kenneth Mutua Gatiri almaarufu Gasigi, Fredrick Muruiki Kiugi aka Papa, Franklin Kimathi almaarufu Dudu Ras, Timothy Kinoti almaarufu Timo na Murangiri Kenneth Guantai almaarufu Tali.

Walinaswa mjini Meru na maafisa wa upelelezi kutoka idara ya Uchunguzi wa Mauaji ya DCI na kuzuiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Nairobi na Kiambu.

Uchunguzi na upasuaji wa mwili wa marehemu katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Marimanti ulibaini kuwa alifariki kwa kunyongwa.

Mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor, aliyefanya uchunguzi huo, alisema Sniper alikuwa na alama kwenye shingo yake na alionyesha dalili za mtu aliyekosa oksijeni.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved