“Hatuanuangi stima!” KPLC yajitetea dhidi ya madai ya kukata stima wakati wa mvua

KPLC imejikuta ikishutumiwa kwa kukata umeme kimakusudi, madai ambayo imekanusha.

Muhtasari

•Kumekuwa na ripoti nyingi za kukatizwa kwa umeme katika maeneo mbalimbali nchini kila mara mvua inaponyesha.

•Kampuni hiyo imefichua kwamba wamechukua hatua za tahadhari kuzuia matatizo ya umeme yasiyotarajiwa.

Image: TWITTER// KPLC

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya, Kenya Power and Lighting Company (KPLC) imejitokeza kujitetea dhidi ya madai ya kusababisha kutatizwa kwa umeme wakati wa mvua.

Kumekuwa na ripoti nyingi za kukatizwa kwa umeme katika maeneo mbalimbali nchini kila mara mvua inaponyesha.

KPLC imejikuta ikishutumiwa kwa kusababisha kukatika kwa umeme kimakusudi, madai ambayo kampuni hiyo sasa imekanusha.

Katika chapisho kwenye Twitter siku ya Jumatatu, kampuni hiyo ilitoa maelezo ya kina ya kile kinachotokea wakati wa mvua inaponyesha na kusababisha kukatika kwa umeme. Walitumia picha zenye maelezo kueleza hali nzima.

“Mvua kubwa mara nyingi huja na upepo mkali. Miti huyumbishwa, matawi yanagusa nyaya, na mara kwa mara matawi huanguka kwenye laini za umeme. Hii husababisha kikatizwa umeme, na kusababisha kukatika kwa umeme,” KPLC ilieleza na kuambatisha taarifa hiyo na picha za kufanya maelezo kueleweka zaidi.

Kampuni hiyo iliyopewa jukumu la kusambaza umeme nchini Kenya hata hivyo ilifichua kwamba wamechukua hatua za tahadhari kuzuia matatizo yasiyotarajiwa.

"Ukiona miti au matawi ya miti karibu na nyaya za umeme, piga *977# au piga 97771 tukushughulikie haraka," kampuni hiyo ilisema.

Image: TWITTER// KPLC
Image: TWITTER// KPLC
Image: TWITTER// KPLC
Image: TWITTER// KPLC
Image: TWITTER// KPLC