Tazama maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme Jumapili- KPLC

KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati utakaokuwa ukifanywa kwenye mitambo.

Muhtasari

•KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Mei 5.

•Baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumapili, Mei 5.

Katika taarifa ya Jumamosi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.Kaunti ambazo zitaathirika ni Uasin Gishu na Homa Bay.

"Habari za jioni. Maeneo yaliyoorodheshwa yataathiriwa na kukatizwa kwa umeme kesho Jumamosi (5 Mei, 2024). Kukatizwa ni sehemu ya matengenezo ya mtandao. Kwa ilani ya mapema, tumia http://bit.ly/31u4jY4. Ili kufikia ratiba ya hivi punde, angalia chini ya tarehe ya hivi majuzi zaidi," KPLC ilisema katika taarifa ya Jumamosi,

Katika kaunti ya Uasin Gishu, maeneo kadhaa yakiwemo CBD, Eagle, Sugar Land Plaza na viunga vyao yatakosa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa tisa alasiri.

Katika kaunti ya Homa Bay, baadhi ya maeneo yakiwemo Nyabola, Mwamba, Jerusalem na viunga vyao yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.