logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kila mwanachama wa Hamas ni mfu, Netanyahu anasema

Idadi ya vifo nchini Israel imefikia 1,200. Zaidi ya watu 1,100 wameuawa huko Gaza.

image
na Davis Ojiambo

Habari12 October 2023 - 05:38

Muhtasari


  • • Rais wa Marekani Joe Biden alisema alikuwa amezungumza na Bw Netanyahu na kuweka wazi kwamba Israel lazima "ifanye kazi kwa kuzingatia sheria za vita".
  • • Bw Biden alisema anaelewa hasira na kufadhaika kwa watu wa Israel lakini akahimiza Israel kuzingatia kanuni za mikataba ya Geneva.
ni miongoni mwa wanachama wa "baraza la mawaziri la vita" la muda

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kila mwanachama wa Hamas ni "maiti" baada ya mkutano wa kwanza wa serikali ya dharura ya nchi yake.

Akiwa pamoja na Netanyahu, kiongozi wa upinzani Benny Gantz alisema pia kwamba Israeli ipo katika "wakati wa vita".

Lakini Rais wa Marekani Joe Biden alisema alikuwa amezungumza na Bw Netanyahu na kuweka wazi kwamba Israel lazima "ifanye kazi kwa kuzingatia sheria za vita".

Idadi ya vifo nchini Israel imefikia 1,200. Zaidi ya watu 1,100 wameuawa kwa mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza.

Bw Biden alisema anaelewa hasira na kufadhaika kwa watu wa Israel lakini akahimiza Israel kuzingatia kanuni za mikataba ya Geneva.

Pia aliionya Iran - ambayo imeafiki shambulio la Hamas - "kuwa makini".

Mapema Jumatano Bw Netanyahu na Bw Gantz walikubaliana kuweka kando uhasama wao mkali wa kisiasa ambao ulikuwa umeongezeka na kusababisha maandamano makubwa.

Bw Gantz aliwaambia raia wa Israel kwamba serikali mpya iliyoundwa "imeungana" na iko tayari "kufuta kitu hiki kinachoitwa Hamas kutoka kwenye uso wa dunia".

Pamoja na Bw Netanyahu na Bw Gantz, kiongozi wa chama cha National Unity Party na waziri wa zamani wa ulinzi, baraza jipya la mawaziri la muda pia litajumuisha Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Yair Lapid, hajajiunga na muungano huo. Hata hivyo, Bw Netanyahu na Bw Gantz walisema katika taarifa ya pamoja kwamba k atatengewe kiti katika baraza la mawaziri la vita.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved