logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu sababu ya mashabiki kuitaka klabu ya Chelsea kumtambua na kumuomboleza Mr Ibu

Mr Ibu alifariki akiwa na umri wa miaka 62 siku chache zilizopita.

image
na Davis Ojiambo

Michezo05 March 2024 - 09:25

Muhtasari


  • • Mkongwe huyo pia alifichua kwamba aliita nyumba yake baada ya uwanja wa nyumbani wa Chelsea, Stamford Bridge.
Mr Ibu

Siku mbili baada ya kifo cha muigizaji mkongwe wa Nollywood John Okafor maarufu kama Mr Ibu kutoka Nigeria, baadhi ya mashabiki wa klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza wameiandikia timu hiyo barua.

Kwa mujibu wa barua hiyo, mashabiki hao wanaitaka Chelsea kumtambua rasmi Mr Ibu na kumuomboleza kabla ya kuanza kwa mechi yao wikendi ugani Stamford Bridge kwa kile wanataka kuwa alikuwa shabiki sugu kwa muda mrefu.

Mashabiki hao waliibua picha za zamani za Mr Ibu akiwa amevalia jezi ya The Blues na pia kufichua mahojiano yake ya awali akizungumza jinsi anavyoithamini timu hiyo katika moyo wake.

Kama ushahidi wa mapenzi yake kwa klabu hiyo ya London Magharibi, Bw Ibu, wakati wa mahojiano mwaka 2017, alifichua kwamba alimpa jina bintiye wa pekee wa kumzaa "Chelsea."

Mkongwe huyo pia alifichua kwamba aliita nyumba yake baada ya uwanja wa nyumbani wa Chelsea, Stamford Bridge.

“Naipenda Chelsea kwa damu yangu yote. Mke wangu alijifungua mtoto wa kike nje ya nchi. Hata kabla sijamuona mtoto wangu, tayari nilimpa jina la Chelsea. Yaani kukuambia…nyumbani kwangu, nyumba yangu inaitwa Stamford Bridge.”

Tazama video ya zamani kutoka kwa mahojiano ya Mr Ibu:


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved