Kalondu: Ndoto yangu ni kupata watoto 5, baba awe na uwezo wa kuwapeleka International School

“Kwa sasa niko single kabisa lakini natafuta mtu ambaye lazima awe bilionea. Kwa vile nimezaliwa peke yangu kwetu, ndoto yangu ni kuzaa watoto 5 lakini baba yao lazima awe ni tajiri mwenye uwezo wa kuwamudu kuishi maisha mazuri."

Muhtasari

• Kalondu alisema kwamba kwa sasa yuko sokoni na anatafuta mwanaume wa kumuoa lakini akaweka vigezo na sifa za mwanamume wa ndoto zake.

Kalondu Musyimi
Kalondu Musyimi
Image: Instagram//Kalondu_Musyimi

Kalondu Musyimi, mwaandishi wa habari za kidijitali kupitia jukwaa la Mpasho amefunguka kuhusiana na maisha yake katika ulimwengu wa kimapenzi.

Akizungumza na Massawe Japanni katika stesheni ya Radio Jambo asubuhi ya Jumatatu, Musyimi aliweka wazi kwamba kwa sasa hana mpenzi, baada ya penzi lake kusambaratika mapema mwaka huu, miezi michache tu kuelekea kuadhimisha miaka miwili pamoja mwezi kesho.

Kalondu alisema kwamba kwa sasa yuko sokoni na anatafuta mwanaume wa kumuoa lakini akaweka vigezo na sifa za mwanamume wa ndoto zake.

Kulingana naye, mwanamume wa kumuoa kwanza lazima awe tayari kwa mapenzi lakini pia awe ni mwenye kunukia utajiri.

Kalondu ambaye ni mtoto wa pekee kwa wazazi wake, alisema ana ndoto ya kuzaa watoto watano, lakini mume wa kuzaa naye sharti awe na uwezo wa kuwaelimisha katika shule za hadhi ya nyota tano.

“Kwa sasa niko single kabisa lakini natafuta mtu ambaye lazima awe bilionea. Kwa vile nimezaliwa peke yangu kwetu, ndoto yangu ni kuzaa watoto 5 lakini baba yao lazima awe ni tajiri mwenye uwezo wa kuwamudu kuishi maisha mazuri ya kuwapeleka ‘international schools’” Kalondu alimwambia Massawe.

Akionesha kuwa yuko makini na hilo la kutafuta mwanaume bilionea, Kalondu alisema yeyote anayejionea kutoshea kweney vigezo hivyo anaweza kumtafuta kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kalondu pia alizungumzia maisha yake ya utotoni na kufichua kuwa hakuwahi ishi na baba yake na alikuja kupata kumfahamu kwa undani akiwa na umri wa miaka 21.

Baba yake anaishi nchini Ujerumani.