Orodha ya waliochaguliwa kwa Tuzo za Grammy 2024 imetoka na mastaa watapigania tuzo hizo za kifahari katika kategoria tofauti.
Rayvanny wa Tanzania na Producer S2kizzy ndio mastaa wawili pekee wa Afrika Mashariki walioingia kwenye orodha hiyo.
Wawili hao wamepata uteuzi wa Grammy 2024 kupitia Albamu ya Maluma ‘Don Juan kupitia Mama Tetema.
Wakati huo huo, Burna Boy wa Nigeria amepata uteuzi mara nne katika tuzo za Grammy 2024.
- “Sittin On Top Of The World” kwa Melodic Rap Performance
- “I Told Them…”kwa Albamu Bora ya Muziki wa Global
- “Alone” kwa Global Music Performance
- “City Boys” kwa African Music Performance
Kwa upande mwingine, Davido ana ameteuliwa kwa vitengo vitatu ambavyo ni;
- FEEL kwaGlobal Music Performance
- UNAVAILABLE kwaAfrican Performance bora
- TIMELESS kwa Global Albumbora
Mastaa hao wa Nigeria waliteuliwa kuwania kipengele cha kwanza cha Muziki wa Kiafrika huku Davido akiteuliwa kwa wimbo wake wa 'Unavailable', Burna Boy kwa 'City Boy', Ayra Starr kwa 'Rush', na Asake kwa 'Amapiano' akimshirikisha Olamide.
Huu ni uteuzi wa kwanza wa Davido, Olamide, Asake, na Ayra Starr katika kile kinachobainisha kutawala kwa muziki wa Nigeria katika bara la Afrika.
Mwimbaji wa Afrika Kusini Tyla pia aliteuliwa katika kitengo cha wimbo wake wa 'Water' ambao ulimpa uteuzi wake wa kwanza.
Vile vile, staa wa Pop wa Nigeria Fireboy pia alipata uteuzi wake wa kwanza wa Grammy kwa mchango wake kwa 'World Music Radio' ya Jon Baptiste ambayo iliteuliwa kwa Albamu Bora ya Mwaka.
CKay pia alipata uteuzi wake wa kwanza kwa uhusika wake katika 'Age of Pleasure' ya Janelle Monae ambayo iliteuliwa kwa Albamu Bora ya Mwaka. Seun Kuti pia anapata uteuzi kwa hisani ya kuonekana kwake kwenye kipindi cha Janelle Monae 'Age of Pleasure.