Harmonize akiri huwa anamsindikiza mpenziwe kwenda chooni kwa jinsi alivyopagawa naye

Konde Boy alifichua kuwa kuandamana na mpenzi wake anapokwenda msalani sasa imekuwa jambo la kawaida kwake.

Muhtasari

•Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alichapisha video iliyomuonyesha akimfuata nyuma mama huyo wa binti mmoja alipokuwa akienda chooni.

•“Msichana mrembo zaidi niliyewahi kumuona duniani.. Kumsindikiza chooni ni swala la kawaida sasa!! Simuamini, sijiamini,” Harmonze aliandika.

Harmonize na mpenzi wake Poshy Queen
Image: HISANI

Mwimbaji maarufu wa bongo fleva Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ameendelea kukiri mapenzi yake mazito kwa mpenzi wake Poshy Queen huku uhusiano wao ukiendelea kuimarika.

Siku ya Jumatatu asubuhi, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alichapisha video iliyomuonyesha akimfuata nyuma mama huyo wa binti mmoja alipokuwa akienda chooni.

Chini ya video hiyo, Konde Boy alifichua kuwa kuandamana na mpenzi wake anapokwenda msalani sasa imekuwa jambo la kawaida kwake.

“Msichana mrembo zaidi niliyewahi kumuona duniani.. Kumsindikiza chooni ni swala la kawaida sasa!! Simuamini, sijiamini,” Harmonze aliandika chini ya video aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram.

Mastaa hao wawili wa bongo sasa wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa miezi kadhaa iliyopita. Habari kuhusu uchumba wao ziliibuka mapema mwaka huu, na kusababisha mijadala mingi na msisimko kwenye mitandao ya kijamii.

Mnamo mwezi Machi, Poshy Queen alionyesha mapenzi yake kwa kumwandikia mpenziwe Harmonize ujumbe mtamu alipokuwa akifikisha miaka 30 leo.

Mwanasosholaiti huyo mrembo alitumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kummiminia Konde Boy maneno matamu huku akitafakari hadithi yao ya mapenzi.

"Kwa mpenzi wangu na rafiki yangu wa karibu       ❤️. Ninaomba kwamba miaka yako ya 30 iwe bora kwako na ufanikiwe kila kitu unachotaka, asante kwa kuniletea mimi na kila mtu karibu nawe furaha na furaha nyingi, NAKUPENDA SANA ADAMU WANGU ❤️.

"Kukuona ukiwa na furaha sana leo kunanifanya nijisikie mwenye furaha sana byb. Keep that smile on your face for me   , God bless you for us daddy 🙏🏽. Happy birthday byb 😘," Poshy Queen aliandika.

Baada ya kuona ujumbe huo, bosi huyo wa Kondegang alijibu; "Kila kitu kwako mpenzi ❤❤❤❤❤ Asante nimebarikiwa kuwa na wewe ❤❤❤❤"

Baada ya habari kuhusu uhusiano wao kujulikana wazi mapema mwaka huu, tetesi ziliibuka kuwa Poshy Queen alikuwa amemtema mcheza santuri wa Harmonize, DJ Seven ili kuwa naye, tetesi ambazo sosholaiti huyo alikanusha akisema hajawahi kutoka kimapenzi na mburudishaji huyo.