Mwanamume aliyeoa kuwafurahisha wazazi wake alia kuchapwa kila siku na mkewe

Jamaa huyo pia alisema kitu kingine ambacho kimemfanya kushindwa kumuacha mkewe licha ya kuwa anamchapa kila siku ni kutokana na ufundi wake kitandani.

Muhtasari

• Baadhi walimshauri kuchaua moja kati ya kujipenda au kuvumilia kichapo akifurahia utundu wa chumbani wa mkewe.

Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Mwanamume mwenye huzuni na mfadhaiko.
Image: Maktaba

Mwanamume mwenye umri wa makamo ambaye amekiri kwamba alioa kwa ajili ya kuwafurahisha na kuwaridhisha wazazi wake sasa Analia kwamba mke aliyemuoa anamchapa kila siku.

Mwanamume huyo ambaye alituma ujumbe wa siri kwa mshawishi katika mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter alimtaka asifichue jina lake lakini akataka ushauri.

Alisema kwamba alioa miama mitano iliyopita ili kuwafurahisha wazazi wake, lakini kwake muda wote huo amekuwa akipambana ndani kwa ndani ya machungu ya maisha kutokana na kipigo ambacho anapokezwa na mkewe karibia kila siku.

“Nimekuwa kwenye ndoa kwa miaka 5 sasa lakini sina furaha katika ndoa yangu. Bado niko katika ndoa hii kwa sababu ya wazazi wangu,” jamaa huyo alisema kwa sauti ya kujuta iliyokosa matumaini.

Japo alikiri kwamba kwa muda mrefu amekuwa akitaka kuachana na mke huyo kwa talaka, mchakato mzima umekuwa mlima wa kuukwea kwani mkewe anajionesha kama mtu mzuri sana kwa wazazi wa mumewe lakini wanapofika ndani wakiwa peke yao, anamgeza mumewe kama mtumwa na kumtia viboko, makofi, mijeledi na mateke.

“Mke wangu ni mzuri kwa wanafamilia wangu, lakini nyumbani kwetu hunichapa kila siku. Ninaona aibu kusema vitu vingine vingi anavyonifanyia,” alisema.

Jamaa huyo pia alisema kitu kingine ambacho kimemfanya kushindwa kumuacha mkewe licha ya kuwa anamchapa kila siku ni kutokana na ufundi wake kitandani.

“Nimekuwa nikitaka kumtaliki lakini yeye ni fundi sana kwa masuala ya kitandani. Nahisi kama nakufa kifo cha polepole katika nyumba yangu,” alimaliza huku akiomba msaada kutoka kwa wanamitandao.

Baadhi ya watu waliotoa maoni katika chapisho hilo walihisi kwamba bwana huyo amechanganyikiwa na yuko katika njia panda kushindwa kuchagua kati vya kujipenda au kupenda ufundi wa kitandani kutoka kwa mkewe.

Walimtaka kuchagua kimoja kama ni kufurahisha ufundi wa kitandani akiendelea kusimangwa na kunyanyaswa au kuchagua kuokoa maisha na afya yake ya akili kwa kuvunja ndoa hiyo ili kuanza safari mpya ya matumaini.

Wewe ungemshauri vipi?