logo

NOW ON AIR

Listen in Live

ILIKUAJE: Nilijua kuwa mimi ni msagaji nikiwa 15 - Imali Lynn

ILIKUAJE: Nilijua kuwa mimi ni msagaji nikiwa 15 - Imali Lynn

image
na

Habari02 October 2020 - 03:01
IMG_9031
Hii leo katika kitengo cha Ilikuaje, Massawe Japanni alikuwa mwenyeji wake mwanadada kwa jina, Imali lynn.

Imali mwenye umri wa miaka 22 ni msagaji na ni kifungua mimba kutoka familia ya watoto watatu.

Je Imali alijuaje yeye ni msagaji?

Nilianza nikiwa mdogo na sikujua nitakuwa msagaji kwani nilipofikisha umri wa adolescent nilikuwa navutiwa na wanawake wenzangu nikiwa na umri wa miaka 15.

Nilikuwa na woga jamii haitanichukulia jinsi nilivyo, nikajaribu uhusiano na wanawake na haikuweza na nikiwa shuleni nilikuwa na uhusiano na nilipopatikana nilifukuzwa.

Imali alifichua kuwa aliwahi fukuzwa shuleni baada ya kushukiwa kuwa na uhusiano na mmoja wa wasichana lakini anasema bahati yake ni kuwa, mamake hakujua sababu yake kufukuzwa kwani ilisemekana alikuwa amepote shuleni.

Vile nilifukuzwa ilikuja na mambo mengi na mamangu hakujishughulisha na mambo ya usagaji bali ni kwa sababu sikulala kwa bweni langu.

Hadi wa leo mama hajui mimi ni msagaji na nimekuja kujua kuwa kina mama hujua kinachofanyika kwa watoto wao.

Anasema kuwa dadake mdogo anajua yeye ni msagaji na hajawahi jaribu kumuingiza katika usagaji.

Je amewahi shiriki mapenzi na mwanaume, na ilikuaje?

Nishawahi shiriki mapenzi na mwanaume ambaye alikuwa mpenzi wangu wa kwanza lakini sikuipenda na nikaamua kujitoa mapema kabla nimvunje roho.

Lynn anasema kuwa huo ulikuwa wakati alikuwa anajitafuta kwani alidhania ni fikra tu lakini hadi sasa ameelewa kuwa anapenda wanawake na hivyo ndivyo alivyo.

Cha kushangaza ni kuwa kuna mtu ambaye ni stalker na amekuwa akimtafuta katika mitandao, kulingana na Lynn huyo mtu humwambia kuwa atamshtaki kwa mamake mambo anayofanya Nairobi huku akimwambia aombewe kwani anafanya mambo ya kishetani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved