Johny alielezea,
Mke wangu alitoka na akaenda na watoto hiyo kitu hunipea stress sana na imekuwa miezi mitatu sasa. Nilitoka mahali tulikuwa tunaishi na nikaenda shagz kiasi na wakati huo sikuwa na kazi.Nikakaa nyumbani for like one month na nikamwacha nyumbani pamoja na wazazi wangu kwani mahali nimejenga ni karibu na wazazi wangu.
Anasema kuwa wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na bado hakuwa ameenda nyumbani kwa Judy ili ajitambulishe, na anasema babake mkewe alimshauri asirudi kwake.
Mara ya mwisho nilizungumza naye ni jana na hakuniambia siku ya kurudi kwani anataka kupumzisha akili.
Kama ilivyo hali siku ya Alhamisi, leo pia patanisho yetu iligongwa mwamba kwani simu ya mkewe Johnny haikujibiwa na ni kama alikuwa amezima simu yake.
Je ni mawaidha yepi unayo kwake bwana Johny?
