Joe Oyoo* Alipata mshutuko ambao hadi sasa bado unamutua hata usingizini baada ya kujipata katika hali ya kutisha . baada ya kuwa katika uhusiano na mpenzi wake kwa mia miwili ,daalili zilikuwa nzuri kwamba walikuwa katika mkondo ufaao kuboresha uhusiano wao hata Zaidi na walikuwa wameanza kuzungumza kuhusu maisha ya baadaye pamoja .
Hata hivyo kiliingia mchanga kitumbua wakati alipogundua vitabia vidogo vodogo ambavypo mwanzoni havikumtisha hasa lakini vilimpa wasi wasi kidogo . Mpenzi wake alianza kuwa muangalifu na simu yake ya mkononi na wakati mwingi aliizima akienda bafuni au hata kuificha . Mwanzoni mwa uhusiano wao hakuna aliyekuwa ameweka nywila katika simu yake ya mkononi na yeyote kati yao angeichukua simu ya mwenzake na kuichakura bila kuwepo hofu ya lolote .
Tabia hiyo ya kuanza kuficha ficha simu na kuizima ilimfanya Oyoo ashuku kwamba palikuwa na jambo baya lililokuwa likifanyika na alichofanya baadaye kilimuacha na majuto na kuathiri uwezo wake kabisa kuwahi tena kumuamini mwanamke yeyote .
Oyoo kupitia rafiki yake anayejua mambo ya teknolojia aliweza kuunganisha mawasiliano ya whatsapp ya simu ya mpenzi wake na tarakilishi bebe yake iliyokuwa nyumbani ili kumwezesha kupata jumbe zote za whatsapp za mpenzi wake na kujua yote kuhusu mawasiliano yake ya simu . Wiki moja baada ya oparesheni hiyo ya kuiduakua simu ya mpenzi wake kufanywa Oyoo alianza kazi yake ya ujasusi na muda sio mrefu alichokipata kilimuacha kinywa wazi lakini pia kilimvunja moyo na tangu hapo hajawahi kabisa kuaini tena mapenzi .
Mpenzi wake alikuwa akizituma picha zake akiwa uchi kwa wanaume wengine! Jambo ambalo lilimkera sana ni kwamba hakuwa tu anazituma picha hizo kwa mtu mmoja bali kwa Zaidi ya wanaume wawili .
‘ Kwa sababu ya heshima iliyokuwepo katika uhusiano wetu ,sikuwahi hata kuitisha picha zake akiwa uchi,lakini nilishangaa kuona kwamba alipiga picha akiwa uchi wa mnyama kuwatumia wanaume wengine …nilikereka sana’ anasema Oyoo .
Akiwa na ushahidi huo alifikiri kwamba mpenzi wake labda angejutia anachofanya na baada ya Oyoo kumhoji kuhusu alichokuwa akifanya ,mpenzi wake alikana kabisa kuwasiliana au kufanya lolote baya na watu wengine . Alianza hata kububujikwa machozi akishangaa mbona Oyoo alikuwa akimshuku na kumshtumu kwa mambo ambayo hakufahamu chimbuko lake . Oyoo hakuamini jinsi mpenzi wake alivyokuwa hana haya kabisa ya kukana kwamba hakuwa akifanya lolote baya licha ya ushahidi ambao alikuwa nao na alipomuonyesha ,mambo yalibadilika
Mpenzi wake huyo alianza kuomba msamaha akisema hatowahi kurudia tena kufanya hayo lakini ilikuwa wazi kwamba ule ndio uliokuwa mwisho wa uhusiano wao na ilikuwa kama muda wote huo ulikuwa umetupwa kwa ajili ya vitendo vya mtu mmoja katika uhusiano wao .
Ndoto za Oyoo kuwahi kuoa na kumuamini mwanamme zilikatikia hapo na hadi wakati huu kumbukumbu zozote kuhusu kujipata katika uhusiano zinamtia machungu kwani anasema miaka mitatu baada ya tukio hilo yungali ana makovu sana na woga wa kumuamini mwanamke .
Oyoo amefika kiwango cha kusema huenda hatowahi kuoa kwa sababu ya alichofanyiwa na mwanamke ambaye alikuwa amempenda kwa dhati .