logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbunge Babu Owino ajitolea kununulia DJ Evolve nyumba

Mbunge huyo wa ODM pia amejitolea kulipa bili zote za hospitali za DJ Evolve.

image
na Radio Jambo

Habari16 December 2021 - 05:46

Muhtasari


•Babu Owino amejitolea kumnunulia nyumba mcheza santuri huyo ambaye alishtakiwa kupiga risasi takriban miaka miwili iliyopita.

•Mbunge huyo wa ODM pia amejitolea kulipa bili zote za hospitali za DJ Evolve.

Babu Owino

Siku ya Jumanne mahakama ilikubali wasilisho la mcheza santuri Felix Orinda (DJ Elvolve) la kumondolea mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino mashtaka ya jaribio la mauaji dhidi yake.

DJ Evolve alikubali kuondoa mashtaka dhidi ya mbunge huyo wa muhula wa kwanza kufuatia suluhisho la nje ya mahakama.

Hata hivyo, Babu atashtakiwa katika shtaka la pili la kujiendesha kwa fujo huku akiwa amebeba bunduki.

Inafahamika katika jhuhdi za kutafuta suluhu ya mzozo nje ya mahakama, Babu Owino amejitolea kumnunulia nyumba mcheza santuri huyo ambaye alishtakiwa kupiga risasi takriban miaka miwili iliyopita.

Katika karatasi za mahakama zilizoonekana na Radio Jambo, mbunge huyo wa ODM pia amejitolea kulipa bili zote za hospitali za DJ Evolve.

Babu amekuwa akijaribu kusuluhisha kesi hiyo nje ya mahakama. Wakili wa familia ya DJ Evolve aliambia mahakama kuwa wako katika hatua za mwisho za mazungumzo. 

Upande wa mashtaka ulithibitisha kuwa mazungumzo yamekuwa yakiendelea kati ya pande hizo mbili.

Mahakama ilisikia kwamba upande wa mashtaka ulifanya mikutano miwili kati ya Babu na Evolve pamoja na mawakili.

Babu Owino alishtakiwa kwa kujaribu kumuua Evolve ambaye alimpiga risasi katika kilabu kimoja jijini Nairobi mnamo Januari 2020.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved