logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Usikubali!" Baba Levo amwambia Kajala kutokubali msamaha wa Harmonize

“Usikubali!” Baba levo alimuandikia Kajala

image
na Radio Jambo

Habari29 March 2022 - 07:47

Muhtasari


Baba Levo amemkataza Kajala kukubali msamaha wa harmonize kurudiana kama wapenzi.

Baba Levo, Kajala Masanja

Baba Levo ni mwanamuziki anayechukuliwa kama ni chawa na kibaraka wa msanii Diamond Platnumz na wasanii wot echini ya lebo ya WCB Wasafi.

Baba Levo amekuwa ni mwandani wqa karibu zaidi wa Diamond kiasi kwamba amechukua ugomvi baina ya Diamond na Harmone kuwa wake sasa dhidi ya Harmonize ambaye ni mbaya wa bosi wake.

Baada ya Harmonize kuandika kwenye instastories zake akimtaka Frida Kajala Kumsamehe na kumrudia ili waendelee kulisukuma gurudumu la mapenzi, baadae Baba Levo alijitokeza wazi na kumtaka Kajala asikubali hata kidogo.

Baba Levo alipakia picha ya Kajala Masanja kwenye Instagram yake na kuifuatisha kwa ujumbe wa neno moja lenye msisitizo wa kutoa amri.

“Usikubali!” aliandika Baba Levo.

Itakumbukwa baada ya habari kuzagaa kwamba Harmonize kipindi kile akiwa katika mahusiano na Kajala alijaribu tena kumvizia mwanawe Paula ambaye wakati huo bado ni mpenzi wa msanii Rayvanny, Baba Levo alimchamba Harmonize kwa maneno makali mpaka kuachia kibao cha kumtukana Harmonize, kibao alichokipa jina baya sana lisiloweza tamkika.

Harmonize alijua wazi kwamba Baba Levo anatumika na mbaya wake Diamond kumpiga vita, na aliyasema haya katika mahojiano aliyoyafanya pindi baada ya kutua kutokea marekani alikokwenda kupiga shoo kwa wiki kadhaa.

Alisema kwamba yeye hana ubaya na Baba Levo, bali chawa huyo wa Wasafi anatumika tu kama zana ya kivita, na mfadhili mkuu wa maneno Baba Levo anayomtupia Harmonize, ni Diamond Platnumz.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved