logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Makampuni ya ulinzi binafsi zina hadi siku 7 kuwalipa masoja viwango stahiki vya mishahara

Bila shaka, hii inakuja kama afueni kwa walinzi wengi wa kibinafasi .

image
na Davis Ojiambo

Habari30 January 2024 - 07:55

Muhtasari


  • • Bila shaka, hii inakuja kama afueni kwa walinzi wengi wa kibinafasi ambao wanajikuta wakitekeleza majukumu yao chini ya mazingira magumu ya kikazi.
Mlinzi akimkagua mkuu wa PSRA, Fazul Mohammed.

Serikali ya Kenya imetoa agizo la makataa ya siku saba kwa makampuni yote ya huduma za ulinzi kuanza kutelekeza nyongeza ya mishahara stahiki kwa walinzi wao ndani ya kipindi hicho.

Katika waraka wa agizo hilo uliochapishwa kwenye ukurasa wa X wa kundi la walinzi binafsi, PSRA, serikali ilitaka makampuni hayo yote kutekeleza agizo hilo na kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha hilo katika kipindi cha wiki moja.

“Kampuni yoyote ya kibinafsi ya ulinzi ambayo itashindwa kuwasilisha nakala iliyotiwa saini na kuidhinishwa ipasavyo ya Ahadi ya Kisheria ndani ya siku 7 zijazo kuanzia tarehe ya agizo hili itafanyiwa mapitio ya kisheria ya hali yake ya usajili na leseni kwa mujibu wa Kifungu cha 32 cha Sheria," Fazul Mahamed, Mkurugenzi Mtendaji na mkurugenzi mkuu, PSRA alisema katika waraka huo.

PSRA iliratibu kima cha chini cha mshahara wa KSh 18,994.08 kwa walinzi, posho ya nyumbani ya KSh 2,849.11 na posho ya saa ya ziada ya KSh 8,156.81, na kusababisha jumla ya malipo ya KSh 30,000.

Katika notisi ya awali, PSRA ilisema kwamba kufuata kima cha chini cha mshahara itakuwa mojawapo ya vigezo vya lazima vinavyotathminiwa wakati wa zabuni.

Bila shaka, hii inakuja kama afueni kwa walinzi wengi wa kibinafasi ambao wanajikuta wakitekeleza majukumu yao chini ya mazingira magumu ya kikazi huku mishahara yao ikiwa ya chini ya kiwango stahiki kisheria.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved