logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto- Hatuna kinyongo na wale waliopigana nasi

DP anayeondoka aliwahi kukiita kituo kwa kile alichokitaja kama kueneza chuki.

image
na Radio Jambo

Uchaguzi05 September 2022 - 17:11

Muhtasari


  • Kabla ya kutoa jibu lake, alimuuliza mwandishi wa habari jinsi kituo hicho kilivyokuwa kikiendelea huku kukiwa na vicheko kutoka kwa watazamaji

Rais mteule William Ruto amesema hana kinyongo na wapinzani wao katika uchaguzi mkuu uliokamilika hivi punde.

Akiongea na vyombo vya habari mjini Karen siku ya Jumatatu muda mfupi baada ya mahakama ya upeo kuidhinisha ushindi wake, Ruto aliahidi waliompigia kura na wale ambao hawakumpigia kura watapata fursa sawa.

Ruto alisema hayo baada ya mwanahabari kutoka Inooro TV kumuuliza swali.

DP anayeondoka aliwahi kukiita kituo kwa kile alichokitaja kama kueneza chuki.

Kabla ya kutoa jibu lake, alimuuliza mwandishi wa habari jinsi kituo hicho kilivyokuwa kikiendelea huku kukiwa na vicheko kutoka kwa watazamaji.

"Na Inooro yuko wapi, marafiki zangu wazuri kutoka citizen wako wapi," aliuliza.

Ruto alisema hayuko kwenye vitabu vibaya na yeyote na kwamba Wakenya wote watatendewa sawa.

"Najua wakati mwingine watu wanadhani watu waliotupigania sana kuwa tuna chuki, hatuna. Sisi ni wanademokrasia na tutashirikiana," alisema.

Mnamo Agosti 4, Ruto alishutumu Inooro na Kameme FM kwa kile alichokitaja kama kueneza ripoti za uwongo.

Alidai kuwa waliokuwa wabunge Njenga Mungai na Joseph Kiuna wamekuwa wakieneza simulizi za vurugu, kupitia vituo hivyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved