Brian Mwebi ,30, kutoka Kakamega alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Lydia Shonda ,27, ambaye alikosana naye wiki jana.
Brian alikiri kwamba amekuwa akimkosea mkewe mara kwa mara katika miaka mitatu ya ndoa yao, jambo ambalo lilimfanya amteme.
"Amenishika na wanawake mara nyingi sana. Nimeona arudi tu kwa nyumba hao watu ni kama wananibomolea boma. Ni wanawake karibu watatu lakini wote sasa nimewablacklist. Najaribu kuongea na yeye arudi anasema ni sharti tuhame mahali tunaishi," Brian alisema.
Aliongeza, "Ni tamaa tu ya macho. Sitarudia tena naomba mnisaidie. Ni kitu nimemfanyia kwa muda na nimefikiria sana nikaamua nimeacha. Karen ndiye alifanya ndoa ikaharibika. Kulikuwa na Osibe na Zawadi. Lakini sasa hivi hata number zao nimefuta kwa simu."
Lydia alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba Brian amekuwa akimkosea mara kwa mara.
"Huyu jamaa alinikosea sana na nilitoka kwa nyumba nikiwa na hasira. Kuna vitu mtu akikosea mara nyingi inakuwa mazoea. Amenikosea sana na warembo," Lydia alifunguka.
Aliendelea, "Kilichofanya nikaondoka, kuna msichana alikuwa maid. Brian alinipatia namba yake ili niongee naye. Nikaongea na huyo msichana, kumbe Brian alikuwa ananichezea tu, akitoka kwa nyumba alikuwa aanaenda kuongea naye. Ikafika wakati huyo msichana akaanza kunifowardia hizo message."
Lydia alibainisha kwamba mwanadada kwa jina Karen ndiye aliyemfanya agure ndoa yake.
Huku akijitetea kwa mkewe, Brian alimwambia, "Nimejua animekukosea sana. Naomba msamaha turudiane. Nimeamua kuweka mambo wazi ili hadi wao wakisikia wajue Brian hayuko hapo.
Lydia hata hivyo aliomba muda zaidi wa kufikiria kabla ya kufanya uamuzi wa kurudi kwenye ndoa hiyo.
"Nilishamsamehe lakini anipatie muda kwa sababu alinikosea sana. Brayo atulie, nitajua vile nitaita watu wangu akuje na wake tuzungumze . Ni lazima athibitishe mbele ya watu kwamba ameacha mambo hayo." alisema.
Brian aliendelea kumshawishi arudi nyumbani huku akimhakikishia kuhusu mapenzi yake makubwa kwake.
"Nataka nikae tu na wewe kwa nyumba mapenzi yote utapata. Nimetambua makosa yangu na naomba msamaha," alisema.