Katika kitengo cha Patanisho kwenye Gidi na Ghost asubuhi, kijana kwa jina Allan Njenga mwenye umri wa miaka 29 kutoka Uthiru alitaka kupatanishwa na mke wake Ann Njeri mwenye umri wa miaka 26
Njenga alisema kwamba ndoa yake ya miaka 7 ilisambaratika miezi 9 iliyopita baada ya mkewe kugundua kwamba alikuwa amewekwa na ‘mumama’.
“Mimi ni dereva wa Uber, sasa ile kutembea kule mtaani kuna wale wanawake wakubwa wenye pesa. Sasa nilipata ‘mumama’ mmoja umri kati ya 38-39 na tukawa marafiki. Siku moja nikasahau kuweka password kwa simu nikiwa nimetoka kazini. Mke akachukua akakagua ndio akapata picha na sms ya huyo mama na wengine kadhaa. Mzozo ukatokea hapo, akachukua watoto, akaita gari na kubeba nguo zake na vitu vya watoto. Kurudi jioni nikapata niko peke yangu…” Njenga alisema.
Alijitetea akasema kwamba ni mtego tu ambao huyo ‘mumama’ alimweka na alikuwa anampa pesa nyingi, na akaanza kumpigia simu bila kutumia mtandao wa Uber na Njenga alipompeleka kwake akiwa amelewa, alihakikisha ameingia kwa nyumba na huyo ‘mumama’ akafunga mlango.
Njenga alisema mkewe alihama walipokuwa wanaishi Uthiru na kwenda kuishi na watoto Kinoo.
Mkewe Njenga alipopigiwa simu, alisema kuwa Allan ako na wanawake wengi – Zaidi ya 3- na akasema alijaribu kumuongelesha ikashindikana.
“Akitokea kazini anakuja kama amelewa, halafu anakuwa anazungumza kwenye simu kama kunionjesha hasira. Mimi nilichoka na yeye, nikachukua watoto na vitu vyangu nikahama. Tabia yake imekuwa kwa Zaidi ya mwaka,” Njeri alisema.
Njeri alisema kwamba mumewe alikuwa anajihusisha na kina mama wakubwa kiumri, Zaidi ya miaka 50.
Allan alijaribu kumuomba msamaha Njeri akisema kwamba ameshaachana na kina mama hao wote lakini mkewe akasema kwamba hataki mambo yake na pia Allan hayuko serious na maisha.
Hata hivyo, mwishowe Njeri alimtaka Allan kumpa muda ili ampe jibu sahihi lakini pia akamtaka afunge safari aende nyumbani kuzungumza na wazazi wa Njeri.