"Tulikosana Sunday lakini kabla ya siku hiyo siku ya Ijumaa nilishika simu yake nikapata ana bet, huwa ana bet lakini wakati huu alikuwa ana bet na fedha nyingi. Mara elfu mbili, nee, tano zote zikiliwa na nikihesabu zote nikapata alikuwa ametumia elfu kumi.Sasa kuamka usiku nikienda nje nikapata alikuwa amepoteza elfu zingine tano, sasa alinipata nikilia kwa kiti na nikamuuliza mbona anatumia fedha za biashara kubet, akasema atawacha hiyo tabia.
Kumbe alikuwa ananidanganya tu na bado alikuwa ana bet. Saturday match ya Champions League alienda na simu ya M-pesa, kumuuliza Sunday yake akaniambia kuna kijana alienda kumuekea fedha aka bet nazo. Kumuuliza akakasirika akanipiga baada ya kukashifu marafiki zake." Alieleza Betty ambaye ameolewa kwa miaka mitatu.
Nicholas alipopigiwa simu alidai kuwa wawili hao walikosania jambo dogo sana na kitu kingine ni kuwa mke wake ana tabia za kukasirika haraka, jambo ambalo halimpendezi.
"Shida ni kuwa anataka niwe na marafiki ambao sio chini ya miaka yangu na unajua mimi ni mwanabiashara na lazima niwe na marafiki wa aina yoyote.
Shida nyingine ni nikibet nikishinda anafurahia na nikipoteza ananikasirikia sasa na anajua kuna kushinda na kushindwa." Alieleza Nic.
&feature=youtu.be
