logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa Hali na Mali: Jacque Maribe amtembelea Itumbi korokoroni

Kwa Hali na Mali: Jacque Maribe amtembelea Itumbi korokoroni

image
na

Burudani02 October 2020 - 02:19
Jackie Maribe
Urafiki wa kufaana . Ndio  taswira inayoweza kueleza uhusiano kati ya mwanahabari Jacque Maribe na Mkurugenzi wa mawasiliano ya kidijitali  katika Ikulu ,Dennis Itumbi . Maribe  siku ya jumatano ‘alirudisha mkono’ kwa kumtembelea Itumbi  katika makao makuu ta DCI wakati alipokamatwa kuhusiana na barua yenye madai ya kuwepo njama ya kumuua naibu wa rais William Ruto.

Itumbi  amekuwa akihudhuria vikao vya kesi ya mauaji inayomkumba Maribe  na mpenziwe wake  wa  zamani Joseph Irungu ,na masaibu yaliomfika  ,jumatano yalitoa  fursa  kwa mwanahabari huyo kwenda kumwona .

Maribe na Jowie wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani katika nyumba za  Lamuria Gardens mwaka wa 2018 . Maribe na Itumbi  wana historia ndefu lakini iliyoghubika usiri kuhusu hali ya uhusiano wao  sasa kwani kwa wakati mmoja  walidaiwa  kuwa wapenzi .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved