logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke kukiri vile aliunga kikundi cha Dini isiyofaa

Mwanamke kukiri vile aliunga kikundi cha Dini isiyofaa

image
na

Burudani02 October 2020 - 11:00
61210353_476693023065651_560232784830568386_n (1)
Mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa hapa mjini Nairobi amekiri kuwa miongoni mwa dini na kuelezea jinsi alivyotumika kushinda nyoyo za watu.

Kilichomfanya kujitokeza na kuongea ni kwa sababu alikuwa ametolewa kutoka kwa mambo hayo maovu na mhubiri mashuhuri T. B Joshua.
Baada ya kupeleka onyo kwenye mtandao wa Facebook, mwanamke huyo aliendelea kuelezea jinsi wanavyotumia vyombo vya habari vya kijamii ili kukuvutia watu
katika mambo hayo alielezea na kusema,
"Mimi nina umri wa miaka 42 lakini ninaye mjukuu. Nilianzishwa katika kikundi hiki nilipokuwa na umri wa miaka 25.
Niliitoa nafsi ya mtoto wangu ambaye alikuwa na miezi 9 kwa wakati huo.
 

Baada ya wiki moja nilianza kuzipata hela amabazo sikujua zilipotoka na kufungua biashara ya viatu ambapo viatu hivyo vya Gikomba vilinipa 400k kwa mwezi. 

 
Nilipata maagizo kutoka mbali kama Lebanon, Marekani, Australia na Dubai, watu walitaka kuvinunua viatu vile.
 
Nilikuwa nikiishi Kawangware lakini baada ya mwezi mmoja nilihamia Kileleshwa, nikanunua gari, na ardhi na kufungua maduka mawili mjini na Mombasa.

 
Baada ya miezi sita mlinzi wangu aliniletea barua iliyokuwa na maelekezo, kwanza nilipaswa kuoga na vitu vingine vilivyoorodheshwa (sitavitaja) na kufanya ibada na damu yangu (sitasema jinsi) na kusafisha nguo zangu na suluhisho nililolifanya na damu yangu.
Nilifanya kama nilivyoagizwa na siku iliyofuata niliondoka nyumbani kama nilivyoagizwa na kwenda kukaa kwenye Archives kuomba pesa (hayo yalikuwa kwenye maelekezo). Niliketi na kuanza kuomba saa 8 asubuhi na watu walianza kunipa fedha na siyo sarafu ila noti.  
Watu waliokuwa wanipatia fedha walikuwa na macho amabayo hayakuwa ya kawaida na waliokosa kunipa walikuwa na macho ya kawaida.
Sherehe niliyoifanya juu ya nguo zangu na kuvaa zinifanya nionekane kuwa mlemavu. Sikuwa na mkono mmoja, nilionekana kuondokana hata
hivyo sikuwa mlemavu.
 

Maelekezo ya pili niliyoyapata yalikuwa ya kuelekea makanisani na kuleta bahati zaidi, furaha na afya.

 
Kabla ya kukaa nilihakikisha kwamba niliwasalimu watu wengi kanisani kwa mkono wangu na kuwasiliana zaidi na watu wengi iwezekanavyo. Kila mtu alitaka kuhusishwa nami.

Biashara yangu iliendelea  kuvuma na nikaupata mwili mzuri sana. Kila mtu alinipenda. Nikawapata marafiki wengi, wanawake na wanaume. Nilikuwa na pesa na kila Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ningekuwa na sherehe kwangu.
 
Baadhi ya marafiki wangu waliishiwa na pesa na wakaanza kunitegemea lakini usaidizi wangu haukuwa wa bure lakini hawakuja hayo. Baadhi ya watoto wao waliopotea na wengine kufa.

Nilikuwa na rafiki wa karibu aliyeitwa Linda. Alikuwa mzuri na alikuwa na ngozi nzuri na laini. Siku moja nilimdanganya na kufanya mapenzi naye na hivyo ndivyo nilivyomtwaa uzuri wake.

Baada ya usiku wetu pamoja, maisha yake yamebadilika na hakujua mbona. Watu hawakupenda, wanaume hawakumtazama mara mbili. Alipoteza kazi yake, na hakuweza kulipa kodi ya nyumba yake. Alikuwa mwembamba. 
 
Niliyabeba mapambo yangu popote nilienda na kumpa mtu yeyote aliyetaka na hivo unakiunga kikundi chetu bila kujua.
Pia tulisababisha ajali kwa wingi."
Soma mengi hapa,
Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved