logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pigo kwa Handshake, Uhuru na Raila Odinga kujitosa siasa za Kibra

Pigo kwa Handshake, Uhuru na Raila Odinga kujitosa siasa za Kibra

image
na

Yanayojiri02 October 2020 - 03:24
unnamed (1)
Uamuzi wa Rais Kenyatta kumuunga mkono mgombeaji wa ubunge McDonald Mariga katika uchaguzi mdogo Kibra una athari kwa "Handshake".

Uhuru Kenyatta alikuwa mwanzoni amejitenga na siasa za Kibra.

Wengi wa wachanganuzi wa siasa walihoji kuwa alihofia kuonyesha msimamo wake kuhusu ubunge wa Kibra ili kuilinda "Handshake."

Soma hadithi nyingine:

Mariga ambaye ni mgeni katika siasa anaonekana kama njama ya Ruto kuonyeshana ubabe wa kisiasa na Raila Odinga.

Hapo jana, wanasiasa na wachanganuzi wa siasa walihoji kuwa sio siri mkataba wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta huenda ukatingizika pakubwa.

Aliyekuwa mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire anasema kuwa siasa za ubabe kati ya ODM na chama cha Jubilee kitadhuru pakubwa "Handshake."

Timothy anahoji kuwa huenda makovu yaliyofunikwa na Handshake yakaibuka tena.

Soma hadithi nyingine:

“Ni jaribio kubwa kuendelea mbele. Itakuwa jambo la kufurahisha kuona jinsi Uhuru na Raila watatatua swala hili."

“Macho yote sasa yapo Kibra kuona jinsi matamshi ya kisiasa yatakavyosemwa. Hii ina maana kuwa semi zote zitakazotokea pale lazima utaifa uwekwe mbele." Alisema Bosire.

Mbunge wa Starehe Charles Njagua anahoji kuwa uamuzi wa Jubilee kuteua mgombeaji kulifanyika kuonyesha kuwa Jubilee na ODM hawapo katika ndoa ya kisiasa.

told the Star that Jubilee's decision to field a candidate was meant to demystify perceptions that ODM and Jubilee were in a political marriage.

“Nafahamu kile ambacho Handshake imefanyia watu wa Nairobi. Handshake sio muungano wa kisiasa kati ya ODM na Jubilee. Sisi ni washindani bado." Aliongeza Bosire.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved