logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+ Video yavuja) Aisha Jumwa akitoa vitisho kwa genge dhalimu Malindi

(+ Video yavuja) Aisha Jumwa akitoa vitisho kwa genge dhalimu Malindi

image
na

Burudani02 October 2020 - 03:47
unnamed-15
Video imevuja katika mtandao wa Twitter ikimwonyesha mbunge wa Malindi Aisha Jumwa akitoa cheche za vitisho kwa genge la vijana linashukiwa kutoka jiji la Nairobi na kuvamia eneo hilo kuzuia vurugu.

Maneno haya ya Aisha yanajiri huku kisa cha mauti cha mjomba kikiripotiwa Ganda katika mkutano wa ODM.

Kufikia sasa haijabainika aliyefyatua risasi hiyo.

Aidha baada ya tukio hilo Aisha ameweza kujitetea,

“Mimi nakumbuka nikifika kwa huo mkutano. Nikishuka tu nilikutana na jamaa mmoja anaitwa Agunga. Na aliniambia mwacheni huyo mama aende atafanya nini na askari wote tunao wote…”

“So mi nikashindwa askari ni utumishi kwa wote na hawawezi kutake side…”

“Nataka niseme ya kwamba kitendo ODM wamefanya sio kizuri…”

“Wale waliopanga mkutano pale wakijua kwamba campaign period ilikuwa imeisha, wao ndio wanatakiwa wakuwe held responsible…” Alifunguka Aisha

Video ya siku chache nyuma inamwonyesha mbunge huyu akitokwa na povu katika mkutano,

https://twitter.com/EngnrDan/status/1184170085558173696

Kinachomkera mama huyu ni genge la wahuni wanaokisiwa kuwa wametumwa kutoka Nairobi kuvuruga amani Malindi,

"Na nyinyi kina mama na kina baba wa Ganda. Hakuna mtu atakuja kututisha hapa..."

"Hii mambo ya ooh wakifanya hivi ooh tutaleta fujo..."

"Kuna vijana walitoka Nairobi. Waliletwa huku na vijana wengi hapa wadogo wadogo sijui kina nani kina Kali..."

"Sijui Governors Voice, sijui ukumbafu gani wanaofanya lakini nataka niwaambie ole wenu..."

"Kwa hivyo hao vijana mlitoka Nairobi na Nationa Youth Leader wa ODM habari zenu nikonazo..."

"Na kama unamangamanga hapa Ganda utuonyesha sisi kifua my friend tutadeal na wewe vizuri..." Anafoka Aisha katika video hiyo

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved