logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilikuwa napigwa na kumwagiwa maji kitandani na mume wangu - Peninah

Nilikuwa napigwa na kumwagiwa maji kitandani na mume wangu - Peninah

image
na

Burudani02 October 2020 - 04:30
Lakini jameni, uwe mume au mke ambaye yuko kwenye ndoa ya mateso na matusi, itakuchukua mda gani kabla uamue kuondoka?

Wengi huvumilia wakiwa na imani kuwa wapendwa wao huenda wakabadilika huku wengine kwa bahati mbaya wakifuatwa na mauti, yote kwa ajili ya mapenzi.

Kisa ambacho unasoma ni cha mwanadada kwa jina Peninah ambaye alijipata taabani mikononi mwa mumewe mkatili. Mumewe alianza kumpiga kila siku bila hata sababu.

Cha kushtua ni kuwa hamna aliyemuamini nyumbani kwao.

Jamaa alikuwa anamuamsha usiku na kumwagia maji kitandani kabla ya kumpa kichapo cha mbwa. Isitoshe alikuwa anacheza nje ya ndoa na rafikiye wa dhati ambaye alikuwa mke wa wenyewe.

Soma usimulizi wake;

Mimi nilikuwa nimeoleka hapa Webuye mahali panaitwa malaha, na kupigwa ndio ilikuwa kazi na nilichoka.

Yeye ni mtu wa bodaboda na alikuwa anatoka asubuhi vizuri jioni akirudi hazungumzi, ukiamka kumpakulia chakula kisha ukirudi kitandani ananimwagia maji kitandani naloa mpaka na godoro yote.

Hapo nikajijazia kuwa labda ametoka mwingine huko town alikotoka, iliendelea hivyo na kuna wakati tukilala kama hajanipiga ikifika saa tisa usiku alikuwa anaamka ananitoa kwa mattress na kuniambia kuwa sijui alikotoa pesa na alivyo nunua na ananiamrisha niamke nilale chini ya simiti.

Nina mtoto mmoja lakini mimba ya pili alinipiga ikatoka, ya tatu ikatoka.

Nilikuwa naenda narudi kwani mbele ya wazazi walikuwa wanaona mimi ndio mbaya kabla ya mwishowe kugundua yeye ndio mbaya.

Ile kitu ilifanya nitoke aki nilikuwa na rafiki yangu ambaye tulikuwa tunauza naye vitu, sasa ile wakati nilikuwa napigwa na kufukuzwa naye alikuwa anarudi kwangu.

Kumbe alikuwa mke wa wenyewe na alipopatikana nyumba ikachomwa na kila kitu kuharibiwa na hapo ndipo kila mtu nyumbani alijua ukweli wote.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved