logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msichana, 10, auwawa baada ya kudhulumiwa na mwili kutupwa

Msichana, 10, auwawa baada ya kudhulumiwa na mwili kutupwa

image
na

Burudani02 October 2020 - 04:36
Mwili wa msichana wa miaka kumi ulipatikana katika eneo la Moisbrige kilomita kadhaa kutoka mto Nzoia baada ya kutupwa na wauaji wasiojulikana.

Mtoto huyo ambaye jina limebanwa alitekwa nyara Jumanne asubuhi na watu wasiojulikana na mwili wake kupatikana ukiwa umetupwa katika eneo la kuvukia reli, kilomita kadhaa kutoka mto Nzoia.

Hili linatendeka wakati ambao wakazi wa eneo hilo wanaomboleza kifo cha mwanafunzi wa chuo kikuu aliyeuliwa kwa kukatakatwa miezi michache iliyopita.

Akizungumzia gazeti la The Star, MCA wa eneo hilo Antony Wabuge alisema kuwa afisa wa polisi kwa hawajaweza kufanya kila wawezalo ili kuwakinga wakazi kutokana na wahalifu.

"We want security in this area to be beefed up, last year Emmy Wanyotta was killed, now an innocent soul has been taken away, what is the function of the police, we want this person arrested as fast as possible," Alisema.

Mjombake msichana huyo Gideon Manyonge alisema kuwa msichana huyo alikuwa anaelekea dukani wakati alipotekwa nyara na kuuawa.

“My niece has died a bitter and painful death, we need justice, as we speak now the security in the area needs to be beefed up and the killers must be arrested for justice to prevail,” aliambia gazeti la the Star.

Mwalimu wake Carolyne Namwalwa alimtaja msichana huyo kama mwenye bidii, mwenye furaha tele na isitoshe mwenye heshima huku akiwataka afisi wa polisi kuhakikisha kuwa wahalifu hao wametiwa mbaroni.

"She was a jovial and good girl who was bright in academics, she was a visionary child." Alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved