Stakabadhi ya mashtaka imesema kwamba mnamo januari tarehe 20 mwezi huu katika jumba la westgate Mall Nyakundi na wengine ambao hawaku kortini walimpunja shilingi milioni 1 Yogesh Pattni ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa Benki ya Victoria Commercial Bank Ltd, kama sehemu ya malipo ya shilingi milioni 17.5 ili kuondoa chapisho waliloweka mtandaoni . Kesi ya upande wa mashtaka ni kwamna Nyakundi aliitisha pesa kama shari la kuondoa chapisho hilo ambalo lilikuwa linaichafulia jina benki hiyo na wafanyikazi .
Wakili wa mlalamishi Kamau Chege amesema Nyakundi anakaidi agizo la mahakama kwani amekuwa akiendelea kuweka mtandaoni taarifa za kuwachafulia jina watu na taasisi mbali mbali . Nyakundi na Mtuhumiwa mwenzake Emmanuel Nyamweya Ongera wameachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni kila mmoja au dhamana mbadala ya shilingi laki tatu pesa taslimu kila mmoja .Kesi hiyo itatajwa Fberuari tarehe 7 .
