Hapa Kenya watu wanadhana mbalimbali kuhusu wanaume kutoka makabila tofuati ya humu nchini. Kuna wale wanaosema ili mwanamke amfurahishe bwanake basi anafaa kufahamu kabila lake ili ajue kama yeye ni stadi ulingoni au ni bwege.
1. Kikuyu
Wanafahamika sana kwa bidii yao ya kutafua pesa lakini licha ya sifa hii wanajulikana sana kwa kuwa wagumu sana kwa pesa zao. Kamau hataharibu pesa zake alizopata kwa jasho kwa mwanamke, ni bora apeleke wanaume wenzake awanunulie kinywaji. Hawana muda mwingi kwa mambo ya mapenzi.
Wakati wa mechi chumbani wanajulikana sana kwa mtindo wa 'kifo cha mende' na ukiwa mrembo anayependa kujaribu mambo mapya 'my friend' uko taabani. Warembo wengi wanasema ujuzi wao chumbani ni hafifu. Kwa hivyo ukiwa mrembo usidhani kwamba Kamau atakupamba na mahaba kama Otieno wako wa zamani.
2. Meru/Kisii
Wanaume kutoka makabila haya mawili ni moto wa kuotea mbali. Wana hasira za haraka na ukicheza na yeyote hatasita kukuadhibu. Hawajui kunyenyekea mbele ya wake zao, uamuzi wao ndio mwisho. Wao ndio vichwa nyumbani mwao.
Lakini licha ya hasira zao, wanajulikana sana kwa bidii yao chumbani na wengi wao ni madereva wa masafa marefu bila kupumzika. Ataendesha trela yako kutoka Kigali Rwanda hadi Nairobi kwa kasi bila kuchoka.
3. Luhya
Wanaume Waluhya waah! ni mambo mbaya. Kama tu wenzao wa Kikuyu, wanaume waluhya ni wagamu kwa pesa. Hawapendi kutumia pesa kwa wake zao, peza zao ni za chakula. Ukiolewa kwa mluhya kuwa tayari kupika ugali kubwa na kukaribisha ukoo wake wote.
Hawa jamaa hata hivyo wanatambulika sana kwa kutembea na mkongojo wa ndovu kila wanapoenda na akishakula 'Obusuma' ole wako ukiwa mke wake utatembea na magoti hawachoki safari ya kwenda Mombasa. Tayarisha tu maji moto na chumvi ukiwa mpenzi wake kuuguza majeraha baada ya safari ndefu ya kukwea mlima.
4. Samburu/Maasai
Hawa wanaume hulka yao ni kuoa wake wengi, kwa hivyo ukiolewa kwa mmoja uwe tayari kuwa na mke mwenza. Wengi wao bado hawajaona mwangaza na huzingatia sana mila zao. Ukiolewa kwa mmoja, kuwa tayari kufuata mila zao.
Atakulazimisha ukeketwe ukiwa mke wake na wanaamini kwamba nafasi ya mwanamke ni jikoni, kuchunga mifugo na kutunza boma. Hii ndio sababu mara nyingi wao huacha wake zao mashambani huku wao wenyewe wakishinda mijini vibarazani.
Hawajui kuonyesha mwanamke mapenzi, akitaka kujitimizia haki zake za kimwili kazi yake ni kumuagiza mkewe asongee akishamaliza anamuacha aende. Wengi wao hawana muda wa kutayarisha wake zao kwa shughuli ya chumbani wao ni 'geuka'.
5. Luo
Wanajulikana sana kwa mapenzi yao moto moto na kudekeza wapenzi wao, lakini mapenzi yao kwa mwanamke hubadilika anapomuoa. Wana majivuno utadhani kwamba wanamiliki nchi, wao ndio matajiri kuliko kila mtu. Wengi wao wamejaza 'mipango ya kando' ambao hudekezwa na kutunzwa kuliko wake zao nyumbani.
Wengi wao wanaishi kwa mikopo ya benki, huku wakiishi maisha ya kifahari lakini anapofariki familia zao huachwa katika maisha ya dhiki. Wengi wao hawapendu kuwekeza kwao maisha ni leo kesho itajipanga.
Ni washambulizi wa kadri chumbani, wengi wao hupenda mbio za 'mita 400', anazunguka uwanja mara moja akimaliza yualala aking'orota.
6. Kalenjin
Wanaume kutoka jamii ya Kalenjini hawajui mapenzi kabisa, ukiwa umeolewa kwa mwanamume mkalenjin utasubiri miaka mingi sana akuite 'darling'. Kwake wewe ni mama watoto hayo majina mengine wachia Wajaluo. Wengi wao wana haya sana kuambia mwanamke kwamba 'nakupenda' atakutumia rafiki yake akueleze hisia zake akitaka kukutongoza.
Wengi wao hawachezi mpira kama kuna mwangaza, atazima taa kwanza kabla ya kutoa ujuzi wake ndani ya blanketi.
Orodha ni refu, lakini kwa sasa warembo uamuzi ni wenu, chagua yule atakayekufaa, kwani kila shetani na mbuyu wake.