logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO:Nilipachika mwanamke mwingine mimba kujua ama niko sawa

PATANISHO:Nilipachika mwanamke mwingine mimba kujua ama niko sawa

image
na

Burudani01 October 2020 - 09:39
Leo katika kitengo cha patanisho bwana Nicholas Kigen,25, alituma ujumbe ili patanishwe na mke wake ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka miwili ilhali walitengana mwaka jana Machi.
"Niliitiwa kazi katika chuo kikuu cha Egerton niliporudi nyumbani nilipata amerudi kwao, nilipompigia simu aliniambia tunaweza kuwa marafiki

Hatujafanikiwa kupata mtoto kwa maana mke wangu ana shida ya kupata mtoto huwa anatumia dawa zakupanga uzazi yaani huwa anatumia dawa ya kienyeji

Nilienda kujipima ili kujua kama niko sawa, nilipachika mwanamke mwingine mimba ili nijue niko sawa." Alieleza Kigen.

Huku akieleza hali yake alisema kuwa hakuenda kwa daktari kwa maana anaogopa sindano, je huo ni uungwana?

Mkewe akizungumza alisema ya kwamba Kigen yuko na bibi tayari.

"Kigen mwenyewe ako na mke alipata baada yangu kuondoka, wacha aendelee na maisha yake mimi mwenyewe na mheshimu lakini mimi si mheshimu

Alikuwa anaenda nje ya ndoa na hata kufanya ngono na mwanamke mwingine." Alieleza Sheila.

Huku bwana huyo akijitetea alisema kuwa anampenda mkewe wake pekeyake, bali mkewe alikana na kumwambia awache uongo.

"Nilikuambia unichue kama dada yako nami nikuchukue kama ndugu yangu, hakuna siku ambayo nitakuamini maishani mwangu sitaki kurudiana naye na sitaki mambo yake tena." Sheila aliongea.

Kwa mengi zaidi tembelea mtandao wetu wa youtube.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved