logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Joey Muthengi aeleza jinsi alikejeliwa kwa miezi 6 baada ya kuonekana katika kipindi cha TPF SS6

Joey alisema kwamba wakati huo alikuwa ametoka mbali kutoka kwa kusongwa na mawazo

image
na Radio Jambo

Burudani16 December 2020 - 07:07

Muhtasari


  • Joey Muthhengi asema kwamba alikejeliwa kwa miezi 6 wakati wa kipindi cha TPF
  • Mwanahabari huyo alisema kwamba aliangalia mahali ametoka na yale yote amepitia
JWNk9kpTURBXy8zZmJjMjNkZDRjYWFkNmI0YWQxZjY1MWY3ZjIxZGIxNi5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

Mwanahabari,muigizaji Joey Muthengi alifahamika sana wakati alionekana na kuwa mmoja wa wasimamizi wa kipindi cha Tusker Project Fame SS6 wakati mwaka wa 2014.

Joey alisema kwamba wakati huo alikuwa ametoka mbali kutoka kwa kusongwa na mawazo akiwa na umri wa chini hadi kuachwa na mpenzi wake.

"Baada ya kuonekana katika kipindi cha Tusker Project Fame,nilikejeliwa sana kwenye mitandao ya kijamii

Nilienda kulia kwa mudaa wa saa moja, kutoka hapo niliamua kurudi tena hata baada ya kukejeliwa kwa muda wa miezi sita, kwa sababu niliangalia mahali nimetoka ni mbali sana 

Niliamua kukaa mbali na mitandao ya kijamii kwa muda." Aliongea Muthengi.

Muthengi alisema baada a kukejeliwa aliongea na watu tofauti ikiwemo ndugu yake na kumwambia kuwa asijali kwa maana anaweza kazi hiyo.

Pia alidai kwamba watu katika kipindi hicho walikuwa wamempenda.

 

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved