logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Afisa mmoja wa usalama afariki huku watatu wakijeruhiwa katika mlipuko wa IED Mandera

Maafisa wa vikosi maalum ni miongoni mwa waliotumwa katika eneo hilo ili kukabiliana na tisho la  Al shabaab .

image
na Radio Jambo

Burudani28 January 2021 - 09:28

Muhtasari


  •   Maafisa wa vikosi maalum ni miongoni mwa waliotumwa katika eneo hilo ili kukabiliana na tisho la  Al shabaab .
  •  Vikosi hivyo siku ya jumapili viliwaua washukiwa wawili wa kundi   Al shabaab na kuwanasa washukiwa watatu .

 Afisa mmoja wa usalama ameaga dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kulipuka kwa bomu la kutgwa ardhini  katika barabara ya Imarjillo-Arabia  huko Mandera .

 Kifaa hicho cha kulipuka kilikuwa kimetegwa pembeni mwa barabara  ili kuwalenga maafisa wa usalama waliokuwa wakipita katika barabara hiyo . maafisa wa usalama waliowasili katika eneo la mlipuko huo muda mfupi baadaye siku ya jumatano wamesema hawakumpata yeyote .

 Mkuu wa polisi wa eneo la kaskazini mashariki  Rono Bunei amesema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo  lakini wamewatuma maafisa Zaidi ili kuimarisha usalama kwa wote katika sehemu hiyo .

 “ Tutaendelea kuwahimiza wananchi katika sehemu hii kushirikiana na idra za usalama ili kuzuia maovu haya . Hakuna anayeweza kueleza jinsi mabomu haya yanavyortegwa  barabarani bila wenyeji kufahamu’  amesema Bunei .

  Maafisa wa vikosi maalum ni miongoni mwa waliotumwa katika eneo hilo ili kukabiliana na tisho la  Al shabaab .

 Vikosi hivyo siku ya jumapili viliwaua washukiwa wawili wa kundi   Al shabaab na kuwanasa washukiwa watatu .

  Hatua hiyo ilijiri baada ya mkutano kati ya wenyeji na maafisa wa serikali  katika eneo la Garissa kuahirishwa dakika za mwisho mwisho.Mkutano huo ulilenga kujadili ongezeko la visa vya mashambulizo ya kundi la Al shabaab .

  


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved