logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kenya kupokea dozi milioni 4.1 za chanjo ya Covid mwezi huu- Covax

Ethiopia  ndio nchi itakayopea kisi kikubwa katika kanaa hii ya dozi  8,928,000.

image
na Radio Jambo

Uchaguzi04 February 2021 - 08:20

Muhtasari


  •  Ethiopia  ndio nchi itakayopea kisi kikubwa katika kanaa hii ya dozi  8,928,000.
  •  Tanzania na  Burundi ndio nchi katika kanda hii ambazo hazijaagiza chanjo hiyo  na hazimo katika orodha ya mataifa yanayotambuliwa na COVAX.

 Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayotarajiwa kupokea chanjo ya Covid 19  kufikia mwisho wa mwezi huu kulingana na COVAX .

 Katika ripoti iliyotolewa siku ya jumatano  Kenya imeorodhesha kuwa miongoni mwa nchi ambazo zitapokea chanjo hioyo  kulingana na utaratibu wa  matumizi ya dharura wa WHO .

 Kenya itapokea dozi   4,176,000  Uganda itapokea 3,552,000 ilhali Rwanda itapokea  dozi    996,000 .

Somalia  itapokea dozi  1,224,000 ilhali sudan itapokea dozi    3,396,000 nayo sudan kusini itapewa dozi   864,000 .

 Ethiopia  ndio nchi itakayopea kisi kikubwa katika kanaa hii ya dozi  8,928,000.

 Tanzania na  Burundi ndio nchi katika kanda hii ambazo hazijaagiza chanjo hiyo  na hazimo katika orodha ya mataifa yanayotambuliwa na COVAX.

COVAX  imesema inataraji  dozi milioni 1.2  za  chanjo ya  Pfizer-BioNTech  kuwa tayari kaika robo ya kwanza ya 2021  baada ya kukamilishwa kwa makubaliano ya utoaji wa chanjo hiyo .

 Chanjo hiyo itapigwa jeki na nyingine kutoka kwa  AstraZeneca/Oxford  ambayo itakuwa tayari kuwekwa chini ya mpango wa COVAX  katika kipindi hicho .

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved