logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nafahamu mpenzi wangu ana mwanamke mwingine lakini hajui kama najua-Mwanamke asimulia

Sababu ya kutomuuliza na kumuacha ni ipi, haya basi soma kwenye usimulizi wake;

image
na Radio Jambo

Burudani26 April 2021 - 11:24

Muhtasari


  • Mwanamke asimulia jinsi anafahamu mpenzi wake ana mpango wa kando
  • Hawakukosea waliposema ukistaajabu ya musa utayaona ya Firauni, kwani visa vya udanganyifu katika uhusiano wa kimapenzi vimezidi kupanda kila kuchao
sad woman

Hawakukosea waliposema ukistaajabu ya musa utayaona ya Firauni, kwani visa vya udanganyifu katika uhusiano wa kimapenzi vimezidi kupanda kila kuchao.

Ndio wengi huwa wanapendana lakini mwishowe upendo unapotelea mbali na kushndwa haswa nini kilitendeka katika uhusiano wao wa kimapenzi.

Kuna wale huwa  wanapatikana wakiwa na mipango ya kando na uhusiano wao kuishia hapo, na kisha wanaachana.

 

Nikiwa katika ziara zangu wikendi iliyopita mwanamke mmoja alisimulia jinsi anafahamu mpenzi wake ana mwanamke mwingine lakini licha ya hayo yote hajamuacha.

Sababu ya kutomuuliza na kumuacha ni ipi, haya basi soma kwenye usimulizi wake;

"Mwaka mmoja uliopita niligundua na kufahamu kuwa mpenzi wangu ana mwanake mwingine,sikumuacha kwa maana kusema kweli  imi nampenda sana na moyo wangu wote, siyuko tayari kumuacha wala kugombana na yeye kwa ajili ya mwanamke huyo

Marafiki zake walinionya umuhusu lakini nilikuwa nimeona upendo wa kweli kutoka kwake,sijawahi pia kumuuliza kwa maana sipendi akikasirika kwa ajili yangu, mpenzi wangu hajui kama nafahamu ana mwanamke mwingine katika maisha yake,"

Pia nilimuuliza kama mwanamume mwenyewe anampenda alisema haya.

"Ndio ananipenda lakini sijui kwanini anafanya vitendo vyenye havistahili licha yangu ya kumpenda sijapanga kumwambia hadi pale ataamua kuniambia ukweli,"

Kwa ushauri wangu mwanamke hujashikiliwa katika uhusiano huo ambao mwanamume wako hakutambui, jitoe na uendelee na maisha usihatarishe maisha yako kwa ajili ya mapenzi.

 

Maoni yako kuhusu usimulizi wa mwanamke huyo ni yapi?azidi kumpenda mwanamume wake au ajiondoe kutoka kwa uhusiano huo?

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved