logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Orodha ya wasanii wa kenya ambao wamefanya collabo na msanii Rose Muhando

Pia ni miongoni mwa wasanii ambao wamefanya collabo nyingi na wasanii tofauti wa nyimbo za injili.

image
na Radio Jambo

Burudani25 May 2021 - 13:04

Muhtasari


  • Orodha ya wasanii wa kenya ambao wamefanya collabo na msanii Rose Muhando
  • Msanii wa nyimbo za injili Rose Muhando ni miongoni mabingwa wa nyimbo za injili kutoka zama za kale

Msanii wa nyimbo za injili Rose Muhando ni miongoni mabingwa wa nyimbo za injili kutoka zama za kale.

Rose anafahamika sana kupitia kwa nyimbo zake zilizopendwa na mashabiki wake na wanamitandao.

Pia ni miongoni mwa wasanii ambao wamefanya collabo nyingi na wasanii tofauti wa nyimbo za injili.

Katika makala haya tutazingatia wasanii wakenya ambao wamefanya collabo na msanii huyo.

1.Betty Bayo

Ni msanii wa nyimbo za injili ambaye anafahamika sana, wiki jana walifanya collabo na msanii Rose Muhando, katika kibao kinachofahamika kama 'unamuwinda nani'.

2.Ringtone

Huwa anajiita mwenyekiti wa burudani ya nyimbo za injili, lifanya collabo na rose muhando katika kibao amcho kinafahamika 'walionicheka' mwaka mmoja uliopita.

3.Size 8

Licha ya janga la corona kuenea sana nchini, wawili hao walishikana na kutoa kibao chao ambacho kilipendwa na mashabiki wao.

Kibao hivho kinafahamika kama 'Vice Versa'.

4. Anastacia Mukabwa

 Ni msanii kutoka kaunti ya Kakamega ambaye alikuwa msanii kutoka Kenya kufanya collabo na msanii Muhando.

Wameimba nyimbo pamoja kama vile kiatu kivue miongoni mwa vibao vingine.

 

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved