logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mshukiwa akamatwa kwa kutapeli wanamitandao malaki ya pesa

'Badman Anchor' amekuwa akitumia kurasa za Instagram kama vile 'Bakcell Apple Store' na 'Netsol Apple store' kuwatapeli watu akijifanya muuzaji mkubwa wa simu aina ya iPhone na bidhaa zingine za kampuni ya Apple.

image
na Radio Jambo

Burudani25 May 2021 - 19:58

Muhtasari


•Mtapeli amekuwa akitumia kurasa za Instagram kama vile 'Bakcell Apple Store' na 'Netsol Apple store' kuwatapeli watu.

• Alikamatwa baada ya watu wengi waliokuwa wameanguka kwenye mtego wake kufikisha malalamishi kwa maafisa wa usalama

mshukiwa

Mwanaume mmoja aliyeshukiwa kuwatapeli Wakenya kupitia mtandao wa Instagram alikamatwa na kuzuiliwa siku ya Jumanne.

Inadaiwa kuwa Victor Maina almaarufu kama 'Badman Anchor' amekuwa akitumia kurasa za Instagram kama vile 'Bakcell Apple Store' na 'Netsol Apple store' kuwaibia watu pesa huku akijifanya muuzaji mkubwa wa simu aina za iPhone na bidhaa zingine za kampuni ya Apple.

Maina alikamatwa baada ya watu wengi waliokuwa wameanguka kwenye mtego wake kufikisha malalamishi kwa maafisa wa usalama. Inadaiwa kuwa mtapeli huyo alikuwa ameibia watu kadhaa malaki ya pesa.

Mshukiwa huyo atafikishwa mahakamani kesho huku akishtakiwa kwa kosa la kupokea pesa kwa kutumia njia ya uwongo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved