logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mmoja afariki, 9 wako hali mahututi baada ya kunywa pombe iliyotiwa sumu Nyahururu

Kumi hao ni miongoni mwa kundi la watu waliohudhuria sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa iliyofanyika Jumapili asubuhi katika baa moja mjini huo

image
na Radio Jambo

Burudani12 July 2021 - 06:51

Muhtasari


•Kulingana na daktari Felix Masongo anayesimamia kitengo cha dharura katika hospitali ya Nyahururu County Referral, tisa wale walifikishwa katika hospitali hiyo Jumapili asubuhi baada ya kuanza kutapika na kuumwa na tumbo.

•Alisema kuwa waliletwa pale hospitalini kwa gari la polisi baada ya kupatikana wakiwa wamelala kando ya barabara katika sehemu mbalimbali za mji wa Nyahururu.

crime scene 1

Mwanaume mmoja ameaga na watu wengine tisa kulazwa hospitali baada ya kukunywa pombe iliyotiwa sumu mjini Nyahururu.

Kumi hao ni miongoni mwa kundi la watu waliohudhuria sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa iliyofanyika Jumapili asubuhi katika baa moja mjini huo.

Akithibitisha tukio hilo, mkuu wa afya katika kaunti ya Laikipia, Daktari Donald Mugoi alisema kuwa watu tisa ambao wamelazwa hospitali wako katika hali mahututi.

Kulingana na daktari Felix Masongo anayesimamia kitengo cha dharura katika hospitali ya Nyahururu County Referral, tisa wale walifikishwa katika hospitali hiyo Jumapili asubuhi baada ya kuanza kutapika na kuumwa na tumbo.

Alisema kuwa waliletwa pale hospitalini kwa gari la polisi baada ya kupatikana wakiwa wamelala kando ya barabara katika sehemu mbalimbali za mji wa Nyahururu.

Hata hivyo, Masongo alisema kuwa hawakuweza kubainisha mara moja kemikali ambayo ilikuwa imetiwa kwenye pombe ama kiwango ambacho kumi hao walikuwa wamekunywa.

Daktari huyo alisema kuwa ni vyema waathiriwa wabakie pale hospitalini kwani kemikali ambayo inatuhumiwa walikunywa inajulikana kusababisha matatizo ya macho baada ya siku tano.

Daktari Mugoi aliagiza wote ambao kuna uwezekano walikunywa pombe iliyoathirika kufika hospitalini ili wapimwe ijulikane hali yao kwani adhari za sumu ile huonekana kati ya masaa 24 na 48.

Baadhi ya waliokuwa wamealikwa katika sherehe ile walisema kuwa mke wa mwenye baa hiyo alikuwa amejifungua.

Kamanda wa polisi maeneo ya Nyahururu, Mary Kiema alisema kuwa uchunguzi ulikuwa umeanza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved