logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanapenda kunitusi na kuniita mzee,'Anerlisa Muigai asema Watanzania wapenda kumkejeli

Kulingana na Anerlisa,  Watanzania daima wanapenda kumdhulumu

image
na Radio Jambo

Burudani19 July 2021 - 12:12

Muhtasari


  • Anerlisa Muigai asema Watanzania wapenda kumkejeli
  • Anerlisa Muigai hatimaye alifungua juu ya aina ya chuki amekuwa akipokea kwenye mitandao ya kijamii 
    Kulingana na Anerlisa,  Watanzania daima wanapenda kumdhulumu na kumuita mwanamke mzee

 Anerlisa Muigai anajulikana na wengi kama mjasiriamali na mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Nero, kampuni inayotengeneza maji ya kunywa.

Anerlisa Muigai amekuwa katika ndoa  na mwimbaji wa Tanzania Ben Pol baada ya muda wawili hao waliachana, jambo ambalo limefanya Anerlisa kupokea kejeli mitandaoni.

Anerlisa Muigai hatimaye alifungua juu ya aina ya chuki amekuwa akipokea kwenye mitandao ya kijamii.

Kulingana na Anerlisa,  Watanzania daima wanapenda kumdhulumu na kumuita mwanamke mzee.

Anerlisa amepuuza kejeli zote hasi na anasema kwamba bado anawapenda Watanzania ambao wamekuwa wakimkejeli na kumshambulia mitandaoni.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Anerlisa amesema licha ya hayo yote angependa watanzania waunge mkono biashara yake.

"Watanzania wanapenda kunidhulumu, na kusema kwamba mimi ni mwanamke mzee lakini hayo yote huwa na ya ruhusu yapitw kwa maana nataka siku moja waunge mkono biashara zetu," Aliandika Anerlisa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved