logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Je ni mambo yapi wasanii wanapaswa kujifunza kutoka kwa msanii Diamond?

Ni msanii ambaye amekuwa katika tasnia ya usanii kwa zaidi ya miaka kumi.

image
na Radio Jambo

Habari30 July 2021 - 13:53

Muhtasari


  • Mambo ambayo wasanii wanapaswa kujifunza kutoka kwa msanii Diamond
Msanii Diamond. (Picha:HISANI)

Staa wa bongo Diamond Platnumz mekuwa akivuma kwa muda sasa,baada ya nyimbo zake kupokea watazamaji zaidi ya milioni moja kwa muda mfupi.

Licha ya Changamoto na kejeli nyingi kutoka kwa wanamitandao, Diamond amekuwa akitia bidii katika kazi yake ya usanii.

Ni msanii ambaye amekuwa katika tasnia ya usanii kwa zaidi ya miaka kumi.

Siku ya Jumanne msanii huyo alitoa kibao ambacho kinafahamika kama Iyo na amabcho kimepikea watazamaji zaidi ya milioni moja.

Sio mara ya kwanza msanii huyo kuvunja rekodi kwa dakika chache.

Je ni mambo yapi au mafunzo yapi ambayo wasanii wanapaswa kujifunza kutoka kwa msanii huyo;

1.Kiki

Diamond amethibitishia wasanii wenake sio lazima msanii atafute kiki iliwimbo wake uweze kuvuma na kupokea watazamaji wengi.

Ni tabia ambayo wasanii wamezoea kutafuta kiki ili kibao au vibao vyao vivume sana mitandaoni.

2.Kazi

Pia amewahakikishia wasanii kupa kazi yao kipaumbele, kwani ndio inawaletea mkata wao wa kila siku.

3.Mashabiki

Diamond ni miongoni mwa wasanii Afrika mashariki wamepokea mashabiki wengi mitandaoni, licha ya hayo yote ameonyesha kwamba ni vyema kuishi na wasanii vizuri, kwani wao ndio wanafanya uenee sana mitandaoni.

4.Pesa

Diamond amekuwa akitumia pesa katika muziki wake, ili kutoa vibao ambavyo vinawapendeza watazamaji, bali sio kutoa kibao ambacho hakiambatani na usanii wako.

Pia ameonyesha kwamba wasanii wanapaswa kushirikiana na wasanii wenzao ili kufaulu katika tasnia ya usanii


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved