Baada ya kuwa jikoni kwa muda hatimaye Otile Brown na staa wa Bongo Darassa wametupakulia kibao moto kweli.
Wawili hao ambao wana weledi mkubwa wa mistari ya muziki na ufuasi mkubwa kote Afrika Mashariki wameshirikiana kuimba kibao 'K.O(Tiktok)' ambacho kimepakiwa mtandaoni wa YouTube alasiri ya leo.
Wimbo huo ambao ni wa kusifia urembo wa wanadada unaanza na sehemu ya Otile Brown kisha kufunga na sehemu ya Darassa.
Hapo awali Otile alikuwa amedai kuwa kulikuwa na vikwazo vilivyofanya kibao hicho kisiachiliwe wiki iliyopita ila kwa sasa wimbo huo unapatikana YouTube.
"Nafahamu tulistahili kuachia wimbo wiki hii ila kuna mambo hayajakuwa sawa.,. na kwa kuwa wiki tayari imeisha tunaomba tutoe wiki ijayo" Otile alisema Ijumaa wiki iliyopita.
Tazama:-
Je maoni yako ni yepi kuhusiana na kibao 'K.O' wameweza au la??
Wimbo huo umepokewa vyema na mashabiki huku ukiwa umetazamwa na zaidi ya watu 30,000 tangu kuachiliwa.