logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Marekani yajitayarisha kwa mashambulio zaidi baada ya milipuko ya jana Kabul

Marekani yajitayarisha kwa mashambulio zaidi baada ya milipuko ya jana Kabul

image
na Radio Jambo

Burudani27 August 2021 - 05:52

Muhtasari


• Jana Alhamisi palitokea shambulio bayakatika uwanja wa ndege wa Kabul nchini Afghanistan lililosababisha vifo vya takriban watu 60.

Makamanda wa Marekani wako macho juu ya hofu ya mashambulio zaidi Kutoka kwa ISIS, pamoja na roketi zinazowezekana au mabomu yanayosafirishwa kwa gari yakilenga uwanja wa ndege wa Kabul, mkuu wa Jeshi la Marekani Frank McKenzie alisema.

Jana Alhamisi palitokea shambulio bayakatika uwanja wa ndege wa Kabul nchini Afghanistan lililosababisha vifo vya takriban watu 60 . Haya ndio ya hivi punde kuhusu shambulio hilo :

  • Tariban watu 60 waliuawa na 140 walijeruhiwa katika milipuko miwili katika uwanja wa ndege wa Kabul - afisa wa afya wa Afghanistan ameiambia BBC
  • Wanajeshi 13 wa Marekani ni miongoni mwa wale waliokufa, Pentagon imethibitisha, katika siku inayoonekana kuwa mbaya zaidi kwa wanajeshi wa Amerika nchini Afghanistan tangu 2011
  • Akijibu shambulio hilo, Rais wa Marekni Joe Biden amewaambia waliohusika : "Tutawasaka na kulipiza"
  • Anaapa pia kumaliza oparesheni ya kuwaokoa watu , lakini amesema kwamba "kumtoa kila mtu nje sio jambo ambalo anaweza kutoa hakikisho "
  • Rais anasema hadi sasa hakuna uthibitisho wa ushirikiano kati ya Taliban na Dola la Kiisilamu, Isis-K ambalo alidai kuwa ndilo lililosababisha shambulio hilo
  • Viongozi wa nchi za Magharibi wamelaani shambulio la Kabul, kwani mataifa kadhaa yanamaliza shughuli zao za uokoaji

Hofu ya mashambulio Zaidi

Makamanda wa Marekani wako macho juu ya hofu ya mashambulio zaidi Kutoka kwa ISIS, pamoja na roketi zinazowezekana au mabomu yanayosafirishwa kwa gari yakilenga uwanja wa ndege wa Kabul, mkuu wa Jeshi la Marekani Frank McKenzie alisema.

"Tunafanya kila tuwezalo kuwa tayari," Jenerali McKenzie alisema, wakati vikosi vya Marekani vikilenga kumaliza kujiondoa kwao Afghanistan.Marekani inharakisha kukamilisha uokoaji kufikia tarehe ya mwisho - 31 Agosti iliyokubaliwa na Taliban.

Rais wa Markani Joe Biden hajazidisha muda wa oparesheni hiyo .Alhamisi jioni alisema kuwa juhudi za uokoaji zitaendelea licha ya mashambulio hayo.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved