logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hii sio njia ya kuomba msamaha-Wahu Kagwi ashtumu Wapi Pay kwa kutetea Paul Ndichu na pacha wake

Wahu alisema kwamba taarifa hiyo sio njia ya kuomba msamaha.

image
na Radio Jambo

Burudani19 October 2021 - 09:28

Muhtasari


  • Wahu Kagwi ashtumu Wapi Pay kwa kutetea Paul Ndichu na pacha wake
wahu 4

Muimbaji Wahu ameshtumu Usimamizi wa Wapi pay juu ya taarifa yao juu ya Eddie na Paul Ndichu waliohusika na kudaiwa kuwachapa wanawake katika hoteli ya  Ole Sereni.

Katika chapisho katika ukurasa wake wa instagram,mama wa wawili alisema kuwa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa kinyume na kile kilichokuwa kwenye video ambayo imeenea Jumatatu.

Wahu alisema kwamba taarifa hiyo sio njia ya kuomba msamaha.

Wahu aliandika;

"Mimi nina hasira sasa hivi !!!!! @ Wapi_pay Ni dhahiri kwamba unasema kwa utata katika taarifa yako! Unasema kwamba wala wewe au waanzilishi wako Eddie na Paul Ndichu wanavumilia unyanyasaji wa kijinsia ... lakini video inaonyesha vinginevyo

Hii sio njia ya kuomba msamaha Hii ni jaribio la chini la kufuta hatia, tabia isiyojibika na ya vurugu

Wapendwa wa kampuni na wanachama wa umma .. Hatuwezi siku hii na umri hukubali aina hii ya haki ya kuwa na hatia na tabia ya kupunguka

Na sheria ya Kenya itaweza," Alliandika Wahu.

"Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, Wapi Pay walisema kuwa Eddie na Paul Ndichu 'walikuwa wanajaribu kutenganisha vita kati ya wanawake wawili.

Kupitia ujumbe ambao ulitolewa kwa wanahabari asubuhi ya Jumanne, Wapi Pay imeomba watu wasite kueneza habari potofu bila msingi wa ukweli kuhusiana na yaliyojiri usiku huo.

"Tunafahamu kuhussu video ambayo inaenezwa mitandaoni kuhusiana na mvurutano uliohusisha Eddie na Paul Ndichu, waanzilishi wenza wa kampuni, katika hoteli moja Nairobi usiku wa Jumamosi.

Tullipata habari hizo bila ladha na zikiwa za kusumbua na tungependa kusema kuwa tabia yoyote inayohusisha ukatili dhidi ya wanawake haziashirii maadili yetu wala ya Eddie na Paul. Tunavyoelewa ni kwamba video hiyo ambayo ni yakutisha  haionyeshi matukio ya kweli ambayo yalitokea usiku huo. Kusema kweli, Paul na Eddie walihusika katika jaribio la kudhibiti vita kati ya wanawake wawili na kujilinda kutokana na wachokozi fulani,"Ilisoma baadhi ya taarifa Wapi Pay.

 

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved