logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Yaishe! achana na DNA lea mtoto,'Akothee amwambia Eric Omondi

Eric alizidi na kusema kwamba alimwambia Jacque wafanye DNA lakini alikataa.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri03 November 2021 - 08:21

Muhtasari


  • Eric alizidi na kusema kwamba alimwambia Jacque wafanye DNA lakini alikataa
  • Huku Akothee akitoa maoni kuhusu vuta ni kuvute ya Eric alimwambia kwamba anapaswa kuachana na DNA na kumlea mwanawe

Drama kati ya Jacque Maribe na mchekeshaji Eric Omondi imezidi, kuvutia baadhi ya watu mashuhuri, huku baadhi yao wakimshauri Eric amlee mtoto wake.

Wanamitandao wengi waliwachwa midomo wazi baada ya Eric kusema kwamba walitumia kondomu walipokuwa wakifanya ngono na Jacque.

Eric alizidi na kusema kwamba alimwambia Jacque wafanye DNA lakini alikataa.

Huku Akothee akitoa maoni kuhusu vuta ni kuvute ya Eric alimwambia kwamba anapaswa kuachana na DNA na kumlea mwanawe.

"Je, nyie watu mna wazo la nini kinahusisha kufanya safari zisizo na kikomo kwenye mahakama ya watoto? Je, unajua aina ya wazazi utakaokutana nao kwenye mahakama ya watoto ๐Ÿ’ช.nyinyi nyote ni watu mashuhuri, mtafedheheka sana ,kupanga laini na wazazi hawana viatu

Eric siku hiyo hautaenda na ulinzi wako ๐Ÿค”๐Ÿค” kwanza hakimu ataona hiyo range rover akushangae vile walinishangaa na V8 nikifukuzana Na baba ya akina Vesha

Eric wachana Na DNA ,sisi wanawake/mama tunaamua nani baba watoto wetu hata kama Sio wako ,tumekuchagua ,wewe lea tu mtoto ni wetu sote

Sikuhitaji kwenda DNA kwa watoto wangu 3 Vesha Rue na fancy , Wote wanafanana na BABA yao

niamini Hadi leo ,jamaa hata haeliwi watoto wake wanakula nini ,wanaishi vipi . Hawa watoto nimewalea kwa mikono yangu ,wakiita watu wasiowazaa Daddy ๐Ÿค”ERIC UNANISIKIA ? @ericomondi," Akotee aliandika.

Aidha alimshauri Maribe awacha kukimbizana na baba mtoto wake, na kulea mwanawe.

"Jacky wewe pia chukuwa kama mzazi ,mpuuze Eric omondi na kuchukua jukumu la maisha ya mtoto wako ,utakuwa na amani , huyu jamaa atakutoa figo ukose pumzi ya kutafuta kuzungumza nawe kama mama asiye na mwenzi wa watoto 5.

Nilipata amani nilipowacha kukimbizana na baby daddies ,mummy roho yangu ilikuwa inatembea kama mchawi ,usiku silali ,mchana sina nguvu 

Ona Sasa hii mbio inatupeleka DNA Tunasumbua mtoto na vitu visivyo stahili . Mummy yaishe! Yaishe !Yaishe !

Mtoto ashajua babake SUPER STAR .MWISHO WA STORY ๐Ÿ’ช MTANIKUMBUKA ๐Ÿ™๐Ÿป

Huyu mtoto atakuja kuwa mtu Mkubwa sanaa ,na nyota mtaumia kea kumuumiza mtoto mdogo Na mambo yenu ya hasira za peni mbili.

kujeni ofisini tusuluhishe maneno haya madogo. @ericomondi wewe ni kipenzi changu ,kai nyathi osiepna asayi ๐Ÿ™๐Ÿป

Umekutana na wakili mbaya ambaye hana hisia kwa mtoto au chochote?."

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoยฉ Radio Jambo 2024. All rights reserved