Naibu Rais, William Ruto amemtumia Kinara wa wa ODM, Raila Odinga ujumbe wa kumtakia heri njema anapoadhimisha mwaka wa 77 tangu azaliwe.
Kupitia ukurusa wake wa Twitter,Ruto amemtakia Kinara waziri huyo mkuu wa zamani miaka mingi duniani.
"Heri ya kuzaliwa Jacom. Ubarikiwe na mengine mengi. @RailaOdinga" Alinakiri Ruto
Happy birthday Jakom. May you be blessed with many more. @RailaOdinga pic.twitter.com/z411U442sh
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) January 7, 2022
Raila anasherekea miaka 77 ya kuzaliwa. Viongozi mbali mbali wamemiminia ujumbe wa kumkatia heri njema siku ya kuzaliwa.
Ujumbe wa Naibu Rais umewashangaza wakenya, kwa sababu ni wiki mbili zilizopita ambapo Ruto alikuwa akisherekea siku ya kuzaliwa na Kinara wa ODM hakumtumia ujumbe wowote.