logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Barack Obama asherekea Michelle kwa ujumbe maluum

Obama alitumia ukurusa wake wa Twitter kuchapisha ujumbe kwa mkewe akimtaja kuwa mwendani wake na mpenzi wa karibu.

image
na

Habari18 January 2022 - 04:39

Muhtasari


•siku ya Jumatatu alitumia ukurusa wake wa Twitter kuchapisha ujumbe kwa mke wae huku akimtaja kuwa mwandani wake na mpenzi wa karibu

Barack Obama na mkewe Michelle Obama

 Aliyekuwa rais wa Amerika Barack Obama siku ya Jumatatu alitumia ukurusa wake wa Twitter kuchapisha ujumbe kwa mkewe akimtaja kuwa mwendani wake na mpenzi wa karibu.

Michelle alikuwa anasherekea siku ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 58. 

Baba huyo wa watoto wawili aliwaeleza wafuasi wake kwamba Michelle si tu mke wake bali rafiki wake wa kufa kuzikana. 

"Heri njema ya kuzaliwa, Michelle. Mpenzi wangu,mshirika  wangu...rafiki yangu mkubwa ... 

Michelle katika picha iliyochapishwa na rais huyo wa zamani wa Marekani, alionekana akimpiga busu mpenzi wake huku wote wakitabasamu na kupendeza pamoja, Michelle   akiwa na kinywaji mkononi.

Vile vile, mashabiki walimtakia Michelle heri njema ya kuzaliwa kupitia sehemu ya maoni ya ukurasa wa Obama.

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved