logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nataka nizikwe na sanduku la kioo- Jose Chameleone atoa maagizo ya mazishi yake

Alitoa wito kwa wasimamizi wowote wa mazishi huko nje ambao wana nia ya kusimamia mazishi yake

image
na

Yanayojiri23 January 2022 - 07:12
BigEye.UG

Mwanamuziki nyota wa Uganda Jose Chameleone ametoa maagizo ya wazi jinsi atakavyozikwa kifo kitakapomjia.

Chameleone haogopi kifo hata kidogo, ikiwa kuna chochote, angependa kufaidika na kifo chake.

Wakati wa mahojiano na NBS, Chameleone alisema meneja wake anajua ni ibada gani angependa kwa dakika zake za mwisho duniani.

Alitoa wito kwa wasimamizi wowote wa mazishi huko nje ambao wana nia ya kusimamia mazishi yake kuu kuwasiliana ili wazungumze kuhusu njia zinazowezekana za kuchuma mapato yake.

Nyota huyo alikuwa na jumba la habari la Uganda, ambalo lilikuwa kivuli kwake. Wanatembea naye kwenye eneo la kuoshea magari huko Ntinda alikokuwa akisafishwa gari lake aina ya Range Rover.

Nyota huyo amerejea hivi punde kutoka Kinshasa ya DRC, ambako alifanya kazi kwa ushirikiano na Koffi Olomide.

Chameleone alisema kuwa mashabiki na vyombo vya habari vinapaswa kucheza muziki wake kwa sasa akiwa hai, na wasisubiri afe ili wabaki wakicheza muziki wake kwa kasi ya juu.

Akimkumbuka marehemu Mowzey Radio aliyefariki miaka 4 iliyopita, Chameleone alisema,

“By the way, mimi nilikuwa shabiki wa kwanza wa Mowzey Radio kwa sababu niliona kipaji chake kisha nikamuonyesha nyie watu... Sio sawa kumkumbuka mtu akikufa unapaswa kuwasherehekea wangali hai

Akiendelea na mipango yake ya mazishi, Chameleone alisema, "Nataka niwe na sanduku la kioo ili kila mtu anione kwa sababu watu wengi watahudhuria mazishi yangu kutoka nchi kadhaa."

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved