logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Hata miujiza huchukua muda kidogo" Muigizaji Celestine Gachuhi athibitisha ujauzito wa mtoto wa kwanza

Mumewe amejivunia ukurasa mpya ambao wamefungua huku akimhakikishia kuwa atasimama naye  kila wakati.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku14 February 2022 - 07:28

Muhtasari


•Gachuhi amepakia picha za  ujauzito wake na kutaja hatua hiyo mpya kama muujiza uliochukua muda kutokea. 

•Habari hizi  zinakuja baada ya  miezi kadhaa ya uvumi wa mashabiki ambao tayari walikuwa wamebaini ongezeko la tumbo la mwigizaji huyo.

Celestine na Kimemia

Mwigizaji wa kipindi cha Selina Celestine Gachuhi na mpenzi wake mwanamuziki Phil Kimemia wamedhihirisha wazi kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

Wanandoa hao wametumia siku ya Valentines kusherehekea mapenzi yao na kutangazia mashabiki kuhusu habari za ujauzito kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Gachuhi amepakia picha za  ujauzito wake na kutaja hatua hiyo mpya kama muujiza uliochukua muda kutokea. 

"Hata miujiza huchukua muda mdogo" Gachuhi aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kimemia kwa upande wake amemsherehekea mkewe kama mwanamke jasiri aliyejawa na upendo, wema na ukarimu mwingi.

Mwanamuziki huyo amejivunia ukurasa mpya ambao wamefungua huku akimhakikishia mkewe kuwa atasimama naye  kila wakati.

"Leo ikiwa ni siku ya Wapendanao, nimechagua kukusherehekea. Wewe ni mwanamke shupavu, mwanamke mrembo, anayejali, mpenzi mwenye upendo, msaidizi na mkarimu. Imekuwa safari nzuri na nimependa kila kitu! Huu ni ukurasa mpya na ghafla unajua tu ni wakati wa kuanza kitu kipya na kuamini miujiza ya mwanzo mpya.  Nitakuwa upande wako wakati wote . Heri za siku ya wapendanao mpenzi Celestine Gachuhi" Gachuhi alisema.

Habari za ujauzito wa Gachuhi  zinakuja baada ya  miezi kadhaa ya uvumi wa mashabiki ambao tayari walikuwa wamebaini kuongezeka kwa saizi ya mwili wa mwigizaji huyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved