Mwanamuziki mashuhuri wa bongo fleva,Ravyanny amemuonya mwahabari wa kituo cha habari cha Wasafi kuacha kufuatilia maisha ya mama wa mtoto wake, Fahyvanny.
Rayvannyy amerejea nchini Tanzania baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya wiki mbili ambapo alikuwa ziarani nchini Dubai kutumbuiza mashabiki wake.
Kupitia ukurusa wake Instastori amesema mwanahabari huyo amekuwa akieneza habari potovu kuhusu Fahyvanny na kumuomba akome kushughulika na mambo yasiyomhusu.
"Juma Lokole, tafadhali usipite mipaka, usivuke mipaka nakuheshimu sana," alisema Rayvanny.
Vivile aliongeza kuwa anapenda kuweka mambo yake nje ya mtandao na hivyo hataki jinsi mwanahabari huyo anazungumzia mahusiano yake hadharani kuwalinganisha vidosho wake wake wawili Paula Kajala na Fahyvanny.
Ninawapea heshima wote, hii sio vita wala sio mambo ya mechi za mpira, sipendi na sitawai kuja kupenda."
Rayvanny amesajiliwa na Lebo ya Wasafi kwa muda mrefu kwa mara ya kwanza amezungumzia mahusiano baina yake na mama wa mtoto wake, hata hivyo siku jana alithihirisha kwamba wangali na uhusiano na Fahyvanny.
